By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mzee Edward Mshogola (76) mkazi wa kitongoji cha Kilundo kata ya New-kiomboi Tarafa ya Kisiriri Wilayani Iramba Mkoa wa Singida Tanzania amemfananisha Mtemi Shuluwa na Mtemi Mkwawa wa Iringa na Mtemi Mirambo wa Urambo Tabora.
Mshogola ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 16, 2019 wakati akiongea na Mwandishi wetu kitongoji cha Kilundo.
Mtemi Shuluwa aliyeishi kijiji cha kisharita kata ya Kinampanda Wilayani Iramba alikua bingwa wa vita za zamani zidi ya maadui zake kutoka maeneo ya Kinampanda, Wembere na Ruruma.
Shuluwa alitumia maarifa na tamaduni kuwaziwia maadui zake wasifike maeneo ya utawala wake.
Akisimulia Mshogola kuwa Shuluwa alikuwa shujaa na mwenye uwezo wa kueleza ujio wa vita.
“Shuluwa alikuwa anaota kuwa vita vinakuja kutokea pande ya mashariki au kaskazini”Alongeza Mshogola
Hali hiyo ilimfanya Mtemi Shuluwa kuwaita waganga wa kiutamaduni kufanya Tawile.
Akifafanua maana ya Tawile, Mshogola amesema kuwa walikuwa wakikamata kuku wanampasua kisha wanaangalia adui yuko upande gani.
Maarifa hayo yalimuwezesha Mtemi Shuluwa kufanya madawa ambayo yaliwafanya maadui zake kutoka Kinampanda, Wembere na Ruruma kutoingia kwenye eneo la utawala wake.
Kipindi hicho kulikuwa na uwadui wa wenyewe kwa wenyewe kutaka kutawala maeneo ambayo mtemi wake atapigwa. Alibainisha Mshogola
Akieleza hatima ya Mtemi Shuluwa, Mshogola amesema Mtemi huyo aliota ndoto na kuwasimulia wajomba zake kuwa “ Mtatawaliwa na mtu mweupe”
Tafsiri na maana ya ndoto hiyo ilikamilika wakati Muingereza alipotuwa katika utawala wa Mtemi Shuluwa huku wakitumia chombo maalumu.
Kwa kuwa maarifa na tamaduni alizozitumia Shuluwa kujificha katika jiwe hilo na kutoonekana na adui yoyote hakuwafanyia wajomba zake walikutwa na Waingereza.
Wakiwa katika utawala wa Mtemi Shuluwa, Waingereza waliwakuta wajomba wa Mtemi huyo na kuanza kuwaadhibu wakiwataka wawaoneshe alipojificha Shuluwa.
Mateso na maumivu yaliwafanya wajomba wa Mtemi huyo kuwaonesha Waingereza mahali alipojificha Shuluwa katika jiwe lake mithili ya kiti, Aliongeza Mshogola
Wazungu hao walimkuta Shuluwa katika jiwe mithili ya kiti lililopo Kisharita inayopakana na kijiji cha Kilundo kata ya New-kiomboi Wilayani Iramba.
Mshogola alisema kuwa Shuluwa alichukuliwa hapo na huenda maarifa na tamaduni zake hakuwachia ukoo wa Shuluwa unaopatikana Kisharita, Kilundo na maeneo mengine wilayani humo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.