Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wamekula kiapo cha uaminifu na kukubali wadhifa wa udiwani ili kuanza majukumu yao mapya katika kipindi cha Miaka mitano 2025-2030.
Uapisho huo umefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Disemba 05, 2025 wakati wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani.
Kiapo hicho kimetolewa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mwanzo Kiomboi Mjini Mhe. Rehema Elisa Uroki ambapo jumla ya madiwani wa kata 20 za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na Madiwani wateule wa viti maalumu 07 wamekula kiapo hicho.
Sambamba na hayo Madiwani walitoa tamko la ahadi ya Uadilifu mbele ya Mwakilishi kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma - Dodoma Ndg. Christian Kapere.
Kikao hicho pia kimeashiria mwanzo wa utekelezaji wa majukumu ya Baraza jipya la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
KIOMBOI, IRAMBA
Postal Address: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Telephone: 026 - 2532253
Mobile: 026 - 2533001
Email: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.