Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Michael Matomora, ametoa wito kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Innocent Msengi pamoja na Waheshimiwa Madiwani kwenda kuwahamasisha Wananchi kuchangia damu kwa hiari kwani kuna hali mbaya katika hospitali ya Wilaya kuwa na upungufu Mkubwa wa damu salama.
Matomora ameyasema hayo kwenye kikao cha Robo ya tatu cha Baraza la Madiwani, kikao kilichofanyika April 30, Mwaka huu katika ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri hiyo.
Matomora akieleza zaidi amesema Jamii ndiyo chanzo cha Damu na hakuna chanzo kingine hivyo kuna umuhimu kwa Wananchi kwenda kuchangia Damu kwenye vituo vyetu vya afya na Zahanati kwani Damu hizohizo zitakuja kuwasaidia wao wenyewe pamoja na Wananchi wengine ambao watahitaji huduma ya damu salama.
" Naomba nitoe taarifa ya hali ya damu salama katika Hospitali yetu na vituo vyetu vya afya kuwa si shwari kwani katika Hospitali yetu ya Wilaya mpaka asubuhi hii Damu salama iliyopo ni chupa 24 tu na tuna chupa 33 pekee za damu ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi "- Amesema.
" Na katika chupa hizo 24 za Damu salama, ina makundi yale manne ya damu A, B, AB na kundi O na haya yana positive na Negative. Damu tuliyonayo ni positive tu. Kundi A tuna chupa 4,peke yake, A+, B+ tuna chupa 3 pekee na O tunazo chupa 7 pekee" Amefafanua DED Matomora.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa, Damu za kundi la negative hakuna hata moja kwani akipatikana mgonjwa au wagonjwa wanaohitaji makundi ya damu hizo itakuwa ni shida, hivyo wito wangu kwa Wananchi ni kujitolea kwa hiari kutoa damu ili baadaye iweze kuwasaidia Wa Tanzania.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.