MAFUNZO KWA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Iramba Magharibi, Ndg. Magesa Aspenas Magesa, amefungua rasmi mafunzo kwa Makarani Waongozaji Wapiga Kura Kwa niaba ya msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Iramba Magharibi leo Oktoba 25, 2025 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Shelui, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Magesa amewataka washiriki wa mafunzo hayo kusoma kwa umakini Katiba, Sheria, Kanuni, Miongozo na Maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na waulize ili waweze kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine pengine yatakuwa na changamoto za kufahamu ili kuwarahisishia katika utekekelezaji wao wa kazi za Uchaguzi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.