MAFUNZO YA WASIMAMIZI WA VITUO NA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Iramba Magharibi, Bi. Magreth Segu, amewataka Wasimamizi wa Vituo pamoja na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura kuzingatia mafunzo wanayopewa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha na ufanisi mkubwa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Oktoba 26, 2025 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Shelui, Bi. Segu amesisitiza umuhimu wa kufuata kanuni na kuzingatia miongozo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao katika vituo vya kupigia kura.
Mafunzo haya yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili, kuanzia Oktoba 26 hadi Oktoba 27, 2025.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.