Hemedi Munga Irambadc
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Monica Samweli ameitunuku pikipiki Jumuiya ya Maji ya kijiji cha Nguvu Mali kata ya Ndago Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Monica ameitunuku pikipiki hiyo leo June 24, 2021 katika hafla fupi iliyofanyika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mjini Kiomboi.
Akiongea na Jumuiya za maji katika hafya hiyo, Monica amewataka wanajumuiya hizo kutumia mafunzo mbalimbali waliyoyapata kuhakikisha wanasimama imara kutoa huduma ya maji katika maeneo yao.
“Niziagize kamati zote za maji kuacha migongano ya kimaslahi na kujikita kutoa huduma ya maji kwa wananchi waliopo katika maeneo yao “ amesisitiza Monica
Katika hatua nyingine amezitaka Kamati za maji kujiamini na kuwa waadilifu katika kutekeleza miradi ya maji iliyopo katika maeneo yao ili kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa kupata maji safi na salama kwa wakati.
Akiongea na jumuiya hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni ameziagiza kamati zote za maji wilayani humo kupanda miti na kusafisha eneo lolote lililochimbwa kisima cha maji.
“Niziagize Jumuiya za Maji kuhakikisha sehemu zilizochimbwa visima mita 60 za kila upande toka katika eneo hilo zinakua safi na zimepandwa miti rafiki” ameagiza Mwageni na kuongeza kuwa
“ Jumuiya za maji zinawajubu wa kuhakikisha zinalinda na kutunza miundombinu na vyanzo vya maji katika maeneo yao.”
Aidha amemuagiza meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya maji kupitia miradi inayotekelezwa ngazi zote.
Pia ameitaka RUWASA kuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa jumuiya zinazofuata kanuni na taratibu za uendeshaji wa jumuiya hizo, hivyo zikaweza kutoa huduma bora na kuikuza miradi hiyo.
Akitoa tarifa fupi ya hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo, Ezra Mwacha amesema kuwa upatikanaji wa maji kwa wananchi umefikia asilimia 59.6 kupitia visima virefu na vifupi na kufanikiwa kujenga skimu 32 zinazotoa hudama ya maji katika vijiji mbalimbali.
Mwacha amesema RUWASA ilipokea 1.3 bilioni kwa mwaka wa fedha uliopita kwa ajili ya miradi ya maji na kufanikiwa kukamilisha mradi wa maji Ujungu, Mgela, Kyalosangi na Songambele.
Pia amesama kwa mwaka wa fedha unaofuata RUWASA imepanga kutekeleza miradi 10, tayari vibali vya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kijiji cha Maluga, Kisiriri na Zinziligi vimeishapatikana na kazi inaendelea.
Kufuatia utekelezaji majukumu mzuri kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uendeshaji wa jumuiya za maji, Mwacha ameizawadia Jumuiya ya Maji Nguvu Mali pikipiki aina ya TVS yenye namba za usajili STL 9283 yenye thamani ya shilingi milioni 3.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maji Nguvu Mali, Kristina Msengi ameishukuru RUWASA kwa kuwapatia zawadi ya pikipiki ambayo itatatua changamoto ya kuwafikia wateja wao kusoma mita na kufanya ukarabati.
Pia amezitaka jumuiya nyingine kufanya kazi kwa ufanisi, uaminifu, uadilifu, uwazi na ushindani wa kujitoa kuitumikia jamii yao.
MWISHO
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Monica Samweli akiwa na Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Ezra Mwacha kulia kwake na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri hiyo Peter John wakifuatilia mada ya Usimamizi wa miradi na utoaji wa taarifa, uendashaji wa Matengenezo wa Mitambo katika utoaji wa huduma za maji na Usimamizi wa fedha na ujuzi wa utunzaji wa vitabu. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya wanajumuiya za maji wakifuatilia kwa makini mada ya Usimamizi wa miradi na utoaji wa taarifa, uendashaji wa Matengenezo wa Mitambo katika utoaji wa huduma za maji na Usimamizi wa fedha na ujuzi wa utunzaji wa vitabu. Picha na Hemedi Munga
Pikipiki alioyoitoa Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Ezra Mwacha, kuizawadia Jumuiya ya Maji Nguvu Mali pikipiki aina ya TVS yenye namba za usajili STL 9283 yenye thamani ya shilingi milioni 3. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.