By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Samweli Shillah amewaasa viongozi walioapishwa kutunza siri za mambo mbalimbali wanayojadili kabla ya kupitishwa.
Shillah ameyasema hayo leo Jumatatu Disemba 2, 2019 wakati wa kuhitimisha zoezi la kuapisha viongozi kata ya ulemo Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba.
Akiongea katika hadhara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amewataka viongozi walioapishwa kubadili tabia walizokuwa nazo kabla ya kuchaguliwa nakuwa na tabia nzuri kwa kuwa wao ni viyoo vya jamii inayowazunguka.
“ Ukiwa kiongozi ulevi wa kupindukia haufai maana sisi ni barua tunayosomwa na wananchi kila siku, lazima tubadilishe tabia zetu,” alisisitiza Shillah
Pia amewataka kutimiza majuku yao ipasavyo kwa kuwa wamepewa zamana ya kuongoza wananchi ambao wamewaamini kuwapa nyazifa hizo.
Akiawaapisha viongozi hao, Hakimu Mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Sydney Nindi amewaeleza viongozi hao kuwa waaminifu kuitumikia vyema na kwa moyo thabiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuhakikisha wanatunza siri za majukumu yao.
Nindi amewasisitiza viongozi hao kuwa watiifu na waadilifu wa sheria za Tanzania na Maadili ya Viongozi wa Umma ili kuleta usawa na maendeleo katika jamii zao.
Pia amewakumbusha kuwa kiongozi ni pamoja na kusikiliza maelekezo wanayopewa na viongozi wao ili kuweza kuwaongoza wananchi kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
Kwa upande wake Kaimu Msimamizi wa Uchaguzi Wilayani humo amewaambia viongozi hao wachape kazi huku akiwabainishia kuwa endapo watakwenda kinyume na maadili, uaminifu na utiifu wa kanuni, taratibu na miongozo, sheria itachukuwa mkondo wake kwa kuwa sheria ni msumeno unaokata kote.
Aidha amewaagiza viongozi hao kuhakikisha wanafunzi wote wa shule za awali, shule za msingi na wale waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanakwenda shule huku akiwataka wawachukulie hatuwa wale watakaokiuka maagizo hayo.
Kuziwia vifo vya akinamama wajawazito na watoto wachanga kwa kuhakikisha wanakuwa na taarifa zao na kuwaelimisha kufika hospitali mapema pindi wapatapo ujauzito.
Viongozi hao wametakiwa kufahamu kuwa serikali inaanzia kwao na sio wilayni, hivyo wameaswa kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na sio kusubiria viongozi kutoka wilayani.
Zoezi la kuapisha wenyeviti wa vijiji, vitongoji, wajumbe mchanganyiko na wajumbe kundi la wanawake lilianza Novemba 30, na kuhitimishwa Disemba 2, 2019 ambapo viongozi wakata 20 wameapishwa.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iramba, Sydney Nindi kushoto aikwa na Kaimu Msimamizi wa uchaguzi katikaki na kulia ni Aro Jimbo wa Uchaguzi wakati wakuwaapisha viongozi mbalimbali. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya viongozi wa vijiji , vitongoji, wajumbe mchanganyiko na wajumbe kundi la wanawake wakiapishwa kuitumikia vyema na kwa moyo thabiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya viongozi wa vijiji , vitongoji, wajumbe mchanganyiko na wajumbe kundi la wanawake wakiapishwa kuitumikia vyema na kwa moyo thabiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha na Hemedi Munga
Hakimu Mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Sydney Nindi akiwaapisa baadhi ya viongozi wa vijiji , vitongoji, wajumbe mchanganyiko na wajumbe kundi la wanawake kuitumikia vyema na kwa moyo thabiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.