Mawaziri sita walioko kwenye kamati maalumu iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassani,Kushughulikia migogoro ya ardhi ikiongozwa na mwenyekiti wake Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mhe. William Lukuvi Imefika wilayani Iramba Mkoani Singida kutoa ujumbe wa Rais juu ya vijiji vitano vilivyokuwa na migogoro na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akiongea hayo mbele ya mkutano mkubwa wa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Kijiji cha Mseko Waziri Lukuvi amesema kwa kipindi kirefu wananchi wa vijiji hivyo kikiwemo Kijiji cha Masimba,Wembere,Nselembwe,Kizonzo na Mseko kuwa hawatahama kwenye vijiji vyao Kama ambavyo ilisemekana hapo awali.
.Aidha Waziri Lukuvi amesema kuwa timu ya wataalamu ipo itakayokuja Singida kuja kuaapanga vizuri lakini hakuna atakayehama katika vijiji hivyo.
Lukuvi ameeleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassani ameagiza kuwa hapana Kiongozi yeyote wa serikali atakayeleta taharuki yoyote kwa wananchi wa vijiji hivyo juu ya agizo lake na kuwataka wataalamu wa serikali wapange maeneo yote ambayo siyo hatarishi ili wananchi wa maeneo hayo waweze kufanya shughuli zao za ufugaji katika eneo Hilo la Wembere kwa vijiji vyote vitano.
Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuacha tabia ya kwenda kuvamia maeneo mengine ambayo yatatengwa kwa ajili ya serikali kuyalinda kwa ajili ya vizazi vijavyo,Kwani kila Kijiji kitawekewa mipaka yake pamoja na alama,hivyo waheshimu.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na utalii mhe. Mary Masanja amewataka wananchi wa vijiji hivyo kuacha tamaa ya kukata miti na kuvamia maeneo hayo na badala yake wayatunze kwa sababu yanatunza maji na wakiyamaliza watakufa njaa.
Aidha Naibu Waziri Masanja amewaasa wananchi hao wayatunze na kuyatumia vizuri maeneo hayo,Hasa wake wenye Ng'ombe,Mbuzi na kondoo wachunge vizuri na maeneo mengine.Waiache serikali iwatunzie kwa ajili ya vizazi vingine .
Naye mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida Alhaji Juma Hassani Kilimba amewataka wananchi wa vijiji hivyo kukaa na kutulia Kama serikali ilivyoelekeza kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani,Kwamba utaratibu mzima utafuatwa na utapangwa vizuri na watambue kuwa serikali hii inawajali wananchi wake,na hawatahama,Pia Chama Cha Mapinduzi ndiyo kilivyoagiza hivyo.
Mwisho.
Imeandaliwa na
Ahmed Makame
0739828236
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.