Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGM uliopo mkoani Geita umefadhili mifuko ya saruji 600 kwa ajili ya Ujenzi wa Bweni la wanafunzi shule ya sekondari Kinambeu kata ya Old Kiomboi wilaya ya Iramba.
Akikabidhi mifuko hiyo ya Saruji kwa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba, muwakilishi wa GGM, Meneja Mwandamizi Miradi na Maendeleo ya Jamii, Wakiri Manase Ndoroma amesema GGM imetenga fedha kwa ajili ya kusaidiana na wananchi.” Kila mwaka tunatenga fedha za kusaidia majanga yanapotokea kwa wananchi, tulipopata barua kutoka kwa viongozi wa wilaya ya Iramba, GGM imeamua kuchangia mifuko 600 ya cement kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi” alisema Wakiri Ndoroma.
Dkt Mwigulu Nchemba amekabidhi mifuko hiyo ya cement kwa Diwani wa kata ya old Kiomboi Mhe Samweli Nasoro (CCM) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni. Na amehaidi kuleta Nondo kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi ya shule ya sekondari Kinambeu.” Ufadhili wa mifuko 600 ya cement ni kwa ajili ya kujenga Bweni la wasichana kutokana kwamba Bweni lilokuwa linatumika liliungua”. Alisema Dkt Ncemba.
Diwani wa kata ya Old Kiomboi Mhe: Samweli Nasorwa (CCM) ameshukuru kwa ufadhili huo wa mifuko 600 ya cement kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita GGM, amesema ujenzi wa Bweni hilo utafanyika kwa weledi zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mwl. Linno Mwageni ametoa Shukrani za Dhati kwa msaada wa mifuko 600 ya cement kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la sekondari kinambeu. “Msaada huu tutautumia kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa bweni hili, Halmashauri ya wilaya ya Iramba inatoa shukrani za dhati kwa kampuni GGM kutoa msaada huo” alisema Mwl. Linno
Wanafunzi wa shule ya sekondari kinambeu wilayani iramba wakiwa na mbunge Dkt Mwigulu Nchemba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.