Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, akiweka jiwe la msingi mradi wa maji katika wiki ya maji Duniani kijiji cha Meli kata ya Old Kimboi.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, amewahutubia viongozi mbalimbali na wananchi walihudhuria uzinduzi huo kuutambua mradi huo kuwa ni wakwao, wanatakiwa wautunze na wafahamu kuwa hili eneo halitaruhusiwa kulima au shughuli yoyote ya kibinadam kufanyika, niwaombe viongozi wa serikali ya kijiji kupanda miti na kubadilisha eneo hili kuwa la hifadhi.
Akisoma kauli mbiu ya wiki ya Maji Kitaifa “Hakuna atakae achwa: Kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wote katika Dunia inayobadilika kitabia ya Nchi”
Kwa kaulimbiu hii tunatarajia mwaka 2020 tutakua juu ya asilimia 80% kama miradi yetu itakwenda vizuri, kila sehemu tuhakikishe tunasimamia usafi wa mazingira, tunapanda miti na tuhakikishe miti hiyo haifi, amesema
Akizungumza katika Wiki ya Maji Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni, amewaomba wenyeviti wa vitongoji na mabalozi kujitokeza siku ya kuunda jumuiya ya maji, wawe walinzi wa hili eneo, mifugo isiingie katika eneo hili ili mradi huu uimarike.
Naye Kaimu Mhandisi wa Wilaya, Athumani Mkalimoto, amesema lengo la mradi huu ni kujenga vituo 12 vya kuchotea maji vyenye jumla ya koki 24, kujenga Mlambo 1 wa kunyweshea mifugo na kuwapatia wananchi wa kijiji cha Meli huduma ya maji safi na salaman na usafi wa mazingira.
Akifafanua gharama za mradi huo, amesema mradi utagharimu shilingi milioni mia nne arobaini na tano laki saba elfu themanini na moja mia tatu hamsini na tano (445,781,355) ambazo zimetolewa na serikali kuu chini ya uongozi wa Mhe, Rais John Joseph Magufuli na Halmashauri kugharamia usimamizi na ushauri wa kitaalam pamoja na kutoa mafunzo, kuelimisha jamii, kuunda na kusajili jumuiya ya watumia maji.
Mradi utawanufaisha zaidi ya wananchi 2,130 kwa kuwapa huduma ya maji safi na salama karibu na makazi wanayoishi ndani ya umbali wa mita 400 kutoka mita 1500, mradi utanufaisha mifugo 3,288 kwa kuwapa maji ya uhakika kwenye mlambo, amesema.
Mhe, diwani wa kata ya Old kiomboi, Samwel, ameonesha furaya yake kwa kupokea mradi huu wa maji katika kijiji cha Meli kwa kuwa utawaepushia magonjwa mengi maana katika kijiji hichi tunategemea maji ya chazo cha Mto Zalala, mradi huu utaleta maendeleo ya ujenzi wa shule na zahanati.
Akizungumza Mwenyekiti wa Huduma ya Jamii, Mhe, Wifredi Jackson Kizanga, amewataka wananchi kuutunza mradi huu mkubwa ambao ni wa kwanza tangia Dunia kuumbwa kuletwa katika kijiji cha Meli haya ni mapenzi ya mungu.
Akihitimisha Mhe, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Samweli Shila, amewataka wananchi kuutumia mradi huu vizuri ili kupata manufaa ya maji kwa kuwa maji ni uhai. Amemtaka mtendaji wa kijiji kuhakikisha miti inamwagiliwa asubuhi na jioni na kila mmoja awe mlinzi wa eneo hili, marufuku kuingiza mifugo.
“Mkurugenzi katika kipimo chakwanza kumpima huyu mtendaji wa kijiji cha Meli ni kusimamia miti hii na anatakiwa aoneshe katika kila taarifa anayowasilisha kwa Mwenyekiti wa Kijiji,” amesema
Akizungumza katika uwekaji wa jiwe la msingi katika Wiki ya Maji, Mzee Msengi mkazi wa kijiji cha Meli amesema walikua wanapata tabu sana kunywa maji machafu, ujio wa Kisima hiki kitawafanya wanywe maji safi na salama.
Kwa upande wake balozi, Elimtomath Samwel Mzile amewataka wakina mama wa kijiji cha Meli wajiunge walipe hiyo pesa ili mradi uwe wao na usipelekwe sehemu nyingine.
Habari na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno P. Mwageni wakwanza kulia akitoka kwenye uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa maji kijiji cha Meli. Wapili kulia ni Meneja wa Misitu Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Bwana Shabani. Picha na Hemedi Munga
Kaimu Mhandisi, Athumani Mkalimoto wakwanza kulia akipokea mkono wa pongezi toka kwa Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula baada ya uwekajiwa jiwe la msingi mradi wa maji kijiji cha Meli. Picha na Hemedi Munga na
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.