Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula,
amefanya ziara leo tarehe 19.03.2019 katika Tarafa ya
Ndago kata ya Ndulungu.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula,
akihutubia katika mkutano wa hadhara amemuagiza
Kaimu OCD Mkuu wa Kituo cha Polisi Ndago,
Rashidi Mchonvu kuwakamata wale wote waliouza
na walionunua Gala la Ushirika nakubomoa nyumba
iliyojengwa katika kiwanja cha serikali.
“Nimetengeneza tume kwenye Wilaya kuangalia na
kuhakiki mali za Ushirika, Ndulungu Gala la
Ushirika mmeliuza, Gala la Ushirika limeliwa,
haya ni maelekezo wala sio ombi, Kaimu OCD
kamata wote waliouza hilo Gala pamoja na
aliyenunua Gala, na eneo la kiwanja libaki
wazi kwenye Ushirika, sitaki maelezo katika
hilo, wote wawajibike, hatuwezi tukachezea mali
za Ushirika na nipate taarifa kabla sijamaliza
ziara yangu kwenye Tarafa hii, hao watu
wamekwisha kamatwa wote na nimepita
nimeangalia sehemu zingine wamejenga ibomolewe
hiyo nyumba, hatuwezi tukachezea maeneo
ya serikali, sio tu la Ushirika na kama
kuna mtu yuko kwenye eneo la serikali
amevamia lazima aondoke,” amesema.
Mhe, Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula
amemuagiza Afisa Tarafa, Gerege Kingu,
kuwashirikisha wazazi na kuwaelemisha maana
halisi ya Elimu bila malipo na kuhakikisha
watoto wote wanakwenda shule na wanakula chakula.
“Simamieni suala la utoro na hakikisheni watoto
wote wanakwenda shule, hakikisheni watoto wote
wanakula chakula shuleni, watoto lazima wale
sio ombi kwenye vijiji vyote,
ninatumia mamlaka kuagiza hili
na sio ombi watoto lazima wale. Hakikisheni
wananchi mnatunza chakula, kulima mazao
mengine yanayokabiliana na hali hii,
mwenye mfugo avune na kununua chakula maana
ni fedhea sana familia kukosa chakula.
Tusimamieni nidhamu, kuheshimiana viongozi
wote wa serikali na hakikisheni mnatekeleza wajibu
wenu kwa kufanya kazi,” amesema
Mhe, Mkuu wa Wilaya amewaambia wananchi kua
tumejipanga kusajili watoto 20,000 wenye umri
chini ya miaka mitano ili wapate vyeti vya kuzaliwa,
mpaka sasa tumekwisha sajili zaidi ya watoto 11,000.
“Simamieni upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa na
hakikisheni mnakitunza maana ukipoteza utalazimika
kutoa garama kukipata ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Amewaomba viongozi kusimamia ugawaji wa
vitambulisho vya mjasiriamali ili viishe, kufanya
hivyo tutakua tunaunga mkono juhudi za Mh Rais,
Daktari John Joseph Magufuli,” amesema
Mhe, Mkuu wa Wilaya amewaambia wananchi kua
Ndulungu bila Rushwa inawezekana na huo ndio
ulinzi na usalama, kwa hivyo wenyeviti wa kamati
ya Ulinzi na Usalama kuanzia ngazi ya kijiji hadi
wilayani kusimamia kutokomeza rushwa.
Naye Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Iramba,
Pachal Lufungulo amewaelimisha wananchi kua
rushwa ni kitu chochote mtu anapewa ili atekeleze
jambo fulani kwa upendeleo, rushwa ni adui wa haki,
rushwa ni kosa la jinai, rushwa ni dhambi na kuwataka
wananchi watakapo ombwa rushwa watoe taarifa
Takukuru, Polisi au kwa Mkuu wa Wilaya.
Mhe, Mkuu wa Wilaya amewaomba wenyeviti wa
vitongoji wote na mabalozi kusimamia na kuimarisha
madaftari ya wageni ili kuahakikisha tunatokomeza
uhamiaji haram.
Akizungumza kwenye mkutano huo kaimu Kamanda
wa Uhamiaji, Insepekta Collins Soka, amesema
Mhamiaji haramu ni raia wa kigeni anayeingia
nchini na kuendelea kuishi nchini bila kufuata
taratibu na sharia za uhamiaji, au anayeingia
nchini kwa mujibu wa sharia za uhamiaji lakini
akaendelea kuishi nchini kinyume na sharia,
kanuni na taratibu.
“Amewataka wananchi kutoa taarifa kwenye ofisi
za Uhamiaji, kituo cha Polisi, au serikali za mitaa
pindi unapohisi kuwepo wahamiaji haramu mahali
popote. Ushiriki wako katika kuwafichua wahamiaji
haramu ni muhimu sana katika kuimarisha ulinzi,
usalama na maendeleo ya nchi,” amesema
Naye Luhende Masangwa mkazi wa Makungi
kijiji cha kipuma Kata ya Ndulungu, amemshukuru
Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Luhahula kwa ziara
yake iliyoweza kuwazindulia jengo la shule shikizi
na kuahidi kuja kulifungua mwaka huu.
Rozi John mkazi wa Makungi kijiji cha kipuma Kata
ya Ndulungu, amefurahi ujio wa Mkuu wa Wilaya,
Emmanuel Luhahula katika ziara yake kwani utasaidia
kuharakisha ujenzi wa shule shikizi iishe haraka
na watoto watu kusomea karibu.
Habari na Hemedi Munga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.