Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Wadau mbalimbali wa maendeleo Wilayani Iramba wamechanga Tsh1.2milioni kusaidia ununuzi wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.
Mchango huo umetolewa leo Jumanne Aprili 28, 2020 mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula alipokutana na Wadau hao wa maendeleo katika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri mjini hapa.
Katika kikao hicho ahadi mbalimbali zimetolewa huku Tsh 6.2milioni zikiahidiwa kutolewa ndani ya siku chache zijazo.
Aidha wadau hao wa maendeleo wametakiwa kulipa pesa hizo kupitia akaunti ya Iramba District Council MIS Deposit 50610000793.
Kufuatia michango hiyo,Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula amewashukuru Wadau hao wa maendeleo kwa kutoa michango yao ili kuisaidia jamii ya Wanairamba.
Pia, amewataka Wadau hao wa maendeleo kuwa mabalozi wa kuwafikishia taarifa Wafanya biashara wote ili waweze kushiriki kuchangia.
“ Niwaombe wafanya biashara mliopo hapa kufikisha ujumbe kwa wengine maana ninataka wafanya biashara wote wa Iramba washiriki kuchangia,” amesisitiza Luhahula
Luhahula amewataka watumishi wa Serikali kuwa waaminifu pindi watakapokua wanakusanya hizo pesa.
“Nikigundua Mtumishi wa Serikali amekwenda kuchangisha kwenye duka akapata elfu ishirini (20,000), au laki moja (100,000) halafu akazila, Ninakuhakikishia Mkurugenzi Mtendaji kuwa Mtumishi huyo hatokua na kazi,” amesisitiza Luhahula
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ibrahimu Mjanaheri amewakumbusha Wadau hao wa maendeleo kutumia nguvu za kiuchumi ili kusaidia kuwalinda wanairamba dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.
“Tuhakikishe tunakua na juhudi za kuiokoa Iramba na Wanyiramba na sisi ambao tuko ndani yake,” amesema Mjanaheri na kuongeza
“Ninataka jambo hili tulifanye la kufa na kupona na sio kubembelezana wakati ni jambo ambalo linaweza kupoteza uhai wa watu na tunanguvu za kujiokoa, lazima tujiokoe.”
Akitoa taarifa pufi mbele ya Wadau hao wa maendeleo, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo, Daktari Hussein Sepoko amesema kuwa watu 170 wamepata mafunzo ya namna ya kupambana na kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona kupitia Wizara ya Afya.
Amefafanua kuwa waliopata mafunzo hayo ni wakufunzi 8 ambao waliweza kuwafundisha Watumishi wote wa Idara ya Afya, Waganga Wafawidhi wa Vituo vya Afya, Madereva wote, Wafagiaji na Walinzi wote.
Naye mmoja wa Wadau hao wa maendeleo, Muwakilishi wa Kampuni ya Sun Shine iliyopo kijiji cha Konkilangi Wilayani humo, ameiomba ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo kuziandikia barua kampuni zote kiwango kinachohitajika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.
Kikao cha Wadau wa Maendeleo kimefanyika kikiwa na lengo la kuhakikisha wanawailinda wananchi kwa kuwa wao ndio wanaonufaika na wananchi, napindi watakapo ugua watawakosa wateja hao.
Na hii ni kwa sababu kuwa ugonjwa huu hauchagui cheo cha mtu , awe Mkuu wa Wilaya, masikini, tajiri, msomi au asio msomi, hivyo kila mmoja aguswe na kuona namna atakavyochaingia.
MWISHO
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Iramba awataka wadau wa maendeleo kutoa nguvu za kiuchumi ili kuisaidia jamii ya Wanyiramba kuepukana na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. Picha na Hemedi Munga
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Daktari Hussein Sepoko akitoa taarifa kwa Wadau wa Maendeleo namna ya kujikinga na maambukizi ya homa kali inayosababishwa na virusi vya corona. Picha na Hemedi Munga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba aliosimama, Pius Songoma akimkaribisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Emmanuel Luhahula kufungua kikao cha Wadau wa Maendeleo kujadili namna bora ya kuchangia upatikanaji wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.