MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI YA TSH BIL. 4.151 WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDA; IMEFUNGULIWA NA MINGINE KUWEKEWA MAWE YA MSINGI NA MWENGE WA UHURU SEPTEMBA 22 MWAKA HUU.
Mwenge wa Uhuru Ulioanza Mbio zake katika Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Ukitokea Mkoa wa Tabora ,Na katika mbio zake katika Wilaya ya Iramba Mwenge wa Uhuru Ukiongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndg Abdallah Shaib Kaimu ameweka jiwe la Msingi shule ya Msingi Ishanga pamoja na Kutembelea mradi wa upandaji miti na hifadhi ya mazingira Kijiji Cha Mseko A.
.Aidha Mwenge wa Uhuru Umezindua Mradi wa Masijala ya Ardhi katika Kijiji Cha Masagi kilichopo Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Mkoani Singida; Na kuvunja Rekodi Katika Mkoa wa Singida Kijiji kuwa na Mradi wa Masijala ya Ardhi Kwa lengo la Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania yaani ( MKURABITA).
Afisa Ardhi Mkuu na mkuu wa Idara ya Ardhi Wilaya ya Iramba Magesa Aspeas Magesa akitoa maelezo Kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kiTaifa Abdallah Shaib Kaimu Amesema kuwa ; mradi huo Utawezeaha Kijiji kutoa Huduma Kwa Ukaribu Kwa Wananchi Wa kijiji hicho pia Kwa Watanzania wote.
Magesa Ameongezea kuwa hii ni kuongeza Tija katika kutoa Huduma za kijiji kuboresha Huduma za Uihifadhi wa Nyaraka za Ardhi na kusogeza Huduma za Ughani za Kilimo, mifugo, Misitu, na Nyuki Katika ngazi ya kijiji.
Amesema h Mradi huo umegharimu Tsh Mil.64 ikiwepo na michango ya Wananchi milioni 3. Ameongeza kuwa matumizi halisi ni Tsh Mil.55.159 .Ambazo kati ya hizo Tsh M3 ni michango ya Wananchi na Serikali kuu ni M.52 .159 na kubakiwa na Salio la Tsh m.8.84. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Abdallah Shaibu Kaimu Uzindua na kuusifia lakini ametoa sku mbili kuhakikisha wamemalizia mapungufu yaliyosalia.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.