By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amewataka waajiriwa wote walioteuliwa kushiriki zoezi la kitaifa kuto kuwa kikwazo cha utekelezaji wa zoezi hilo kwa wakati.
Mwageni ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 23, 2019 wakati wa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliofanyika katika ukumbi mkubwa wa Halmashauri hiyo.
Akiongea katika mafunzo hayo, Mwageni amewataka Maafisa waandikishaji wasaidizi na BVR Kit Operator kutotumia uzoefu ambao mara nyingi hupelekea kuharibu kazi kwa kuwa kazi hii sio ya mwaka ule ni mpya.
“Usije ukafananisha mwaka ule nilifanya hivi, hata mashine ni tofauti na zinazotumika mwaka huu.” Aliongeza Mwageni
Maafisa waandikishaji wasaidizi na BVR Kit Operator wametahadharishwa kutokuaribu kazi wala kuiba kifaa chochote katika vifaa ambavyo watapewa kufanyia kazi hiyo.
“Tahadhari ! mnakwenda kufanya kazi muhimu, kazi ya kitaifa ambayo Taifa limegaramia garama kubwa, msiwe sehemu ya kuharibu kazi , mtakabidhiwa vifaa vya kufanyia kazi, mvitunze hivyo vifaa, usiingie tamaa ya kifaa chochote ulichokabidhiwa, utakabidhiwa kwa maandishi na utarudisha kwa maandishi, ukiharibu utawajibika kisheria” Alisema Mwageni
Aidha amewataka maafisa hao kutambua kuwa kila kazi inamsemaji na kuwataka wasiwe wasemaji mahala ambapo hawatakiwi kusema ispokuwa kwa maelekezo.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Iramba na Mkalama, Makwaya Charles amewataka maafisa waandikishaji wasaidizi na BVR Kit Operator kuwa waadilifu na waaminifu katika kazi hiyo.
Aidha amewaambia viapo vyao walivyoapa viwapelekee kuyatekeleza yale yaliyomo ndani ya viapo hivyo huku akitolea mfano wa kuapa kwa kutumia katiba ya nchi.
“Unapoapa kwa katiba ya nchi, huapi kuheshimu ganda la juu, unakula kiapo kuyatumikia na kulinda yaliomo ndani ya katiba kwa maana yake tume imekuamini sana kulitekeleza jukumu hilo.” Alisema Charles
Amewaomba watumishi hao kutunza siri na kuwasiliana na watu sahihi huku akiwataka kutokuwapa taarifa wasio husika katika kazi hiyo.
Akiongea katika semina hiyo kwa niamba ya washiriki wote Mwenyekiti wa semina hiyo, Mtendaji wa Kata ya Ndago , Ndugu Gerege amemuhakikishia mgeni rasmi kuwa watatekeleza majuku hayo kwa mujibu wa maelekezo ambayo wanapatiwa na wakufuzi wao. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya kituo wakifuatilia mafuzo wakati wa semina ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya kituo wakifuatilia mafuzo ya vitendo ya BVR Kit Operator wakati wa semina ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.