By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amefungua rasmi zoezi la kuwaapisha viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mwageni amefugua uapishaji huo leo Jumamosi Novemba 30, 2019 kata ya Shelui Tarafa ya Shelui Wilayani humo.
Ambapo wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji, wajumbe mchanganyiko na wajumbe kundi la wanawake wameapishwa kiapo cha uaminifu na kile cha utii na uadilifu.
Katika ufunguzi huo Mwageni amewaambia viongozi walioapishwa kuwa wanatakiwa kuainisha rasilimali, fursa zilizopo na changamoto ndani ya kitongoji na namna ya kutumia rasilimali zilizopo kutatua changamoto zao ambapo ndio utekelezaji wa ugatuaji wa madaraka ulioboreshwa unaotaka mipango yote ya maendeleo kila watu wanaanza kujipanga kadri wanavyoishi.
Huku akiwataka wawe viongozi wenye kuhamasisha shughuli za maendeleo kwa sababu itasaidia kupatikana ajira kwa vijana wetu.
“ Msiwe viongozi wa kubeza shughuli za maendeleo mkawe viongozi wa kuhamasisha shughuli za maendeleo” alisisitiza Mwageni
Hata hivyo Mwageni amewakataza viongozi hao kuingia mikataba na wawekezaji waliopo katika maeneo yao bila kushirikisha uwongozi wa wilaya ili uweze kuwasaidia kuingia mikataba yenye tija.
Amewataka viongozi hao kusimamia makusanyo ya serikali za vijiji na kuhakikisha pesa zinakwenda benki katika akaunti za vijiji.
Akiwaapisha viongozi hao Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Shelui, Egdius Byabajuka amewataka kuwa waaminifu, watiifu na waadilifu wa majukumu yao huku akiwakataza kuvunja ndoa za wananchi wao kwa kuwa chombo chenye mamlaka ya kuvunja ndoa ni mahakama na sio wao.
Naye msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iramba Magharibi, Salumu Sefu amewaagiza wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata kusimamia zoezi la makabidhiano kati ya viongozi walioapishwa na wale waliomaliza muda wao ili waanze kazi mara moja kwa kuwa tayari wameishaapishwa.
Kwa upande wake Afisa wa kuzuwia na kupambana na rushwa wilayani humo (TAKUKURU ), Benjamini Masyaga amewaelimisha viongozi hao kujiepusha na vitendo vya rushwa huku akiwataka kuwa mtsari wa mbele kutoa taarifa kila wanapoona viashiria vya rushwa katika jamii yao.
Aidha amewataka kufahamu miradi na pesa yoyote inayoletwa katika vijiji vyao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuwataka kusoma mapato na matumizi.
Uapishaji huo umefanyika katika kata ya Shelui, Mgongo, Ntwike, Tulya na Mtoa kwa tarafa ya Shelui wakati tarafa ya Ndago umefanika katika kata ya Mukulu, Ndago, Mbelekese na Kaselya.
Huku ukitarajiwa kuendelea jumapili kwa kata zilizobakia katika tarafa ya Shelui na ndago na kuhitimishwa siku ya juma tatu katika tarafa ya Kisiriri na Kinampanda.
Uchaguzi wa serikali za Mitaa ulifanyika Novemba 24, 2019 na kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo na Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo ambapo Chama cha Mapindizi (CCM) kiliibuka na ushindi wakishindo kwenye vijiji, mitaa na vitongoji.
Afisa wa Kuzuwia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Benjamini Masyaga akiwaelimisha viongonzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji walioapishwa leo kujiepusha na rushwa na kutoa taarifa ya viashiria vya rushwa TAKUKURU. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya viongonzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji wakiapa kiapo cha uaminifu na kile cha utii na uadilifu mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Shelui, Egdius Byabajuka. Picha na Hemedi Munga
Picha ya pamoja kati ya viongonzi wa Vijiji, Mitaa na Vitongoji na wasimamisi wa uchaguzi ngazi ya wilaya ya Iramba baada ya kuapishwa. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.