Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amesikiliza kero na changamoto mbalimbali za watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida na kuzitolea majibu.
Mwageni amezungumza na Watumishi hao katika kikao kilichofanyika leo Ijumaa Januari 31, 2020 katika Ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Katika kikao hicho Mwageni amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo kutenga muda kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za watumishi waliopo katika mamlaka zao na kuzitolea majibu huku akiwaamuru kuzifikisha kwake zinaposhindikina kwa utatuzi zaidi.
Amewasisitiza watumishi hao kutunza nyaraka za serikali na kuto kuwa na kopi au kutoka nazo nje ya Halmashauri hiyo.
“Ninawasisitiza watumishi wenzangu hasa mkirejea sheria inayohusu nyaraka ni makosa kuwa na nyaraka zilizokwisha ingizwa katika utaratibu wa Halmashauri,” amebainisha Mwageni
Pia amekemea taiba ya watumishi kubeba mafaili yao kwani kunachukua majukumu ya watu, hivyo amemuagiza Afisa Utumishi wa Wilaya hiyo B’hango Lyangwa kushughulika na watu hao kwa mujibu wa taratibu na kanunu za utumishi wa umma.
“Ninakuagiza Afisa Utumishi kuwachukulia hatua watumishi hao, nanyi mnaohusika na mafaili ni marufuku mtumishi kubeba faili lake,” aliongeza Mwageni
Akiongelea suala la mawasiliano amewakumbusha Watumishi hao kuwa msemaji katika Idara au Kitengo ni Mkuu wa Kitengo au Idara na msemaji wa taasisi ni Mkuu wa Taasisi.
Hivyo amekemea Mtumishi yoyote asie kuwa Mkuu wa Idara au Kitengo kutoa taarifa kwani kufanya hivyo ni kutengeneza migogoro.
Hata hivyo amewataka Watumishi hao kuwa makini na magrupu mbalimbali ya mitandao ya kijamii na kuacha tabia ya kufowadi taarifa yoyote usiokua na uhakika nayo.
“ Nimarufuku kutuma barua yoyote kwa njia ya magrupu na haipendezi Mtumishi wa Halmashauri hii kukutwa na makosa ya kimtandao,” amekataza Mwageni
Vile vile amewataka kuwa na tabia ya kuheshimiana, kuthaminiana na kuzibiti hasira, dharau na mihemko yao wakati wakiwahudumia wananchi au wao kwa wao.
Aidha amewaagiza Wakuu wa Idara na Vitengo kufanya tathimini ya Watumishi waliochini yao kutoa huduma kwa kulinda muda.
Pia amewaagiza Wakuu hao kuweka vibao vinavyotoa taarifa kuwa ni marufuku kupita eneo la Halmashauri ifikapo saa kumi na mbili jioni, siku za sikukuu na siku za mapumziko.
Kufuatia kua karibu na Makao Makuu ya Nchi, Mwageni amewataka Watumishi hao kutumia fursa ya kutumia ardhi kulima mazao mbalimbali na kuyapeleka Dodoma.
Kufanya hivyo kutawawezesha Watumishi hao kukuza uchumi wao kihalali.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti Uadilifu katika Halmashauri hiyo, Abraham Mosi amewatahadharisha Watumishi wa Idara ya Elimu Sekondari, Elimu Msingi, Afya , Maliasili na Ardhi na kitengo cha Manunuzi kujiepusha na viashiria vya rushwa.
“Ninawaomba Watumishi wenzangu kujitahidi kua wema na waadilifu wakati wote,” amesisitiza Mosi
Awali akitoa kero yake mbele ya Mkurugenzi huyo, Elieza Kipimo amewaomba Watumishi wenzake kuepuka tabia ya kuuliza posho pindi wanapotakiwa kufanya kazi fulani.
Naye Mtumishi mwingine kutoka Kitengo cha Manunuzi, Omari Jumanne amewaomba Watumishi wenzake kuhuisha uhusiano wao kazini hasa pale panapojitokeza matatizo yalio nje ya taratibu za kiutumishi.
Pia Mtumishi kutoka Idara ya Mifugo na Uvuvi, Deogratius Isagala amewaomba Wakuu wa Idara na Vitengo kua na fotokopia na printa katika ofisi zao kwani kufaya hivyo kutasaidia kutunza nyaraka za serikali.
Isagala amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na siku ya familia au siku ya iramba ( Family day or Iramba day) itakayokusanya Watumishi wote, wale, wanywe wacheze, wabadilishane mawazo na kutambulisha watumishi wapya, kupitia mfumo huo Watumishi wote watafahamiana na kudumisha upendo kati yao.
Watumishi mbalimbali wa Makao Makuu wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.