Hemedi Munga Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amefanya ziara ya kukagua ukamilishaji wa Maabara 9 za kemia zinazokamilishwa katika shule 9 Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwageni amefanya ziara hiyo leo Ijumaa Julai 23, 2021 wakati alipotembelea baahdi ya shule 9 kukagua ukamilishaji wa maabara hizo zilizopo Wilayani hapa.
Akiongea na kamati ya manunuzi ya Shule ya Sekondari Kidaru, Mwageni amezitaka kamati zote za manunuzi katika wilaya hiyo kuwa na tabia ya kujadili miradi ya maendeleo katika vikao vyao vya kiutawala ili iwasaidie kuweza kubaini kwa haraka kama kuna changamoto na kuweza kuitafutia ufumbuzi kwa muda stahiki.
Aidha amewataka viongozi wote ambao katika maeneo yao wanamiradi ya maendeleo wanapokuwa wamepata changamoto ya usafiri wa kusafirishia vifaa vya ujenzi kufika Halmashauri mapema kupata gari litakaloweza kuwarahishia usafirishaji wa vifavaa kupeleka katika maeneo yao ya miradi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Godfrey Mwanjala amesema kuwa maabara hizo zimekamilika kwa kiwango bora kinachohitajika na tayari Serikali imekwisha leta vifaa vya maabara hizo.
Mwanjala amesema kuwa Serikali kuu ilileta takriban Tst 210 milioni kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara za kemia.
Amefafanua kuwa maabara hizo zimekamilishwa katika shule ya Sekondari New Kiomboi, Sekondari ya Kisiriri, Sekondari ya Kidaru, Sekondari ya Mgongo, Sekondari ya Mukulu, Sekondari ya Mbelekese, Sekondari ya Mtoa, Sekondari ya Ushora na Sekondari ya Kyengege.
Pia ametowa wito kwa walimu wote kuhakikisha wanatumia weledi wao wakisaidiwa na uwepo wa maabara pamoja na vifaa vilivyopo kuhakikisha wanafunzi wananufaika kwa kupata taaluma bora itakayowawezesha kufaulu vizuri katika mitihani yao ya mwisho.
Akiongea na Mwandishi wetu Mkuu wa Shule ya New Kiomboi, Amadeus Kiduu amesema kuwa maabara ipo tayari na itaanza kutumika wakati wowote tokea sasa.
Naye Mwalimu wa shule ya Sekondari Kidaru, Leonard Mgenzi ametumia fursa ya ziara hiyo kuwaomba viongozi kuendelea kutoa elimu kwa kamati zote zinazosimamia miradi mbalmbali ili wapate ujuzi wa kusimamia kwa umakini na usahihi wa miradi hiyo.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amefanya ziara ya kukagua ukamilishaji wa Maabara 9 za kemia zinazokamilishwa katika shule 9 Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Kulia ni Mkuu wa Shule ya New Kiomboi na kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule ya New Kiomboi, Ndugu Nkololo. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akiwa na baadhi ya Wakuu wa Idara pamoja na kamati mbalimbali za moja kati ya shule alizozitembelea wakati wa ziara hiyo. Picha na Hemedi Munga
Moja kati ya Maabara 9 zinazokamilishwa Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida kwa fedha iliyotoka Serikali kuu takribani Tsh 210 milioni. Picha na Hemedi Munga
Moja kati ya Maabara 9 zilizojengwa katika shule 9 Wilayani Iramba Mkoa wa Singida ziko tayari kuanza kutumika kwa kuwa zimekamilka kwa ubora unaohitajika . Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.