Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amefanya ziara ya kushitukiza kukagua ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Misigiri inayojengwa kijiji cha Misigiri kata ya Ulemo.
Linno amefanya ziara hiyo leo Jumatano Machi 11, 2020 katika eneo ambalo linajengwa stendi mpya ya mabasi ya Misigiri kijiji cha Misigiri kata ya Ulemo Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Ujenzi wa Stendi mpya ya mabasi ya Misigiri umefika hatua ya umwagaji wa kifusi kilichosambazwa na kushindiliwa katika maeneo ambayo mabasi yatakua yanapita.
Kasi ya ujenzi huo imeongezeka kufuatia agizo alilolitoa Machi 5 mwaka huu akiwa na Kamati ya Fedha Mipango na Utawala ya Halmashauri hiyo,
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tyosela kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kuongeza kasi.
Halikadhalika barabara ya kuchepuka wakati wa kuingia na kutoka katika stendi hiyo imeanzwa kuchongwa.
Stendi mpya ya mabasi ya Misigiri inatarajiwa kutumia takribani Sh11.81 milioni kukamilisha ujenzi huo.
Mpaka sasa ujenzi umepita hatua ya lenta ambapo zaidi Sh5.9 milioni zimetumika kujenga choo chenye matundu matatu ya wanaume na matundu matano ya wanawake.
Aidha wametakiwa waliopewa vibanda kulipa Sh50,000 ili kukamilisha ujenzi kwa wakati na kwamba wale wote watakochelewa kulipia watanyanganywa vidanda na kuwapa wale watakaokuwa tayari kulipia kwa wakati.
Katika eneo hilo kunatarajiwa kujengwa jengo la kupumzikia abiria, kibada cha polisi na hoteli kubwa.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba akielekeza jambo wakati akikagua ujenzi wa stendi ya mabasi kijiji cha Misigiri wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni wakwanza kulia akifafanua jambo kuhusu ujenzi wa stendi ya mabasi kijiji cha Misigiri Wilaya Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.