Hemedi Munga, Irambadc
Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni ametoa ahadi ya machine ya kubunia vifaa mbalimbali ikiwemo pawatila kwa mbunifu Benson Mkoma wa kata ya Mtekente Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Mwageni ametoa ahadi hiyo leo agast 5, 2020 wakati alipokuwa akiongea na Wakulima na Wajasiriamali waliofika katika banda la Wilaya ya Iramba Jijini Dodoma katika siku ya sherehe za maonesho ya Wakulima Nane Nane mwaka huu.
“Ndugu zangu Wakulima na Wajasiriamali ni muda sasa wa kutumia teknolojia ya namna ya kupanda na kumwagilia kwa kutumia umeme wa jua kwa sababu vinasaidia kupata mavuno mengi” amesema Mwageni na kuahidi kuwa
“Kwa upande wa Mbunifu wa Pawatila kuna ofa ya machine ya kubunia vitu mbalimbali nitakayokupa bure ili kazi yako iwe kubuni vitu mbalimbali na kuvisajili ili uweze kuwa unalipwa na kushirikikishwa katika miradi mingine.”
Amewataka Wakulima na Wajasiriamali hao pindi watakaporudi Iramba kuwa wajumbe wazuri wa kufikisha ujuzi na maarifa waliyo yapata kupitia maonesho ya Nane Nane zilizokua na kauli mbiu isemayo “Kwa maendeleo ya kilimo, ufugaji na uvuvi chagua viongozi bora mwaka 2020”
Katika hatua nyingine wakulima na Wajasiriamali hao wamepatiwa mafunzo ya namna ya kulima mazao ya alizeti, mtama, kabeji, nyanya, maharage ya kisasa, pilipili hoho na mahindi kisasa kwa sababu ya kupata tija kupitia kilimo na kubadilisha hali zao za maisha katika uchumi wakati.
Akitoa mafunzo hayo mtaalam toka kampuni ya Export Trade Group iliyopo Jijini Arusha, Abdul Abassy amewataka Wakulima hao kuwa makini na wadudu wanaoharibu mimea yao hasa majani kwa kuwa majani yanamchango mkubwa kwenye mimea kwa uvunaji bora.
“Wadudu wanapoingia wanaweza athiri Majani ya mimea na majani ndio kila kitu kwenye mmea,hivyo wadudu wanapokuwa wameharibu majani na afya ya mimea inakuwa ni mbovu” amesema Abassy na kuongeza kuwa
“Ndugu Wakulima mnatakiwa kuzingatia upandaji wa kisasa na matumizi sahihi ya mbolea kwa hatua mbalimbali za mmea ili mazao yaweze kustawi vizuri.”
Akijibu swali la mmoja wa Wakulima hao aliotaka kujua kuwa hekari moja inakuwa na mashimo mangapi na kwa kilo ngapi unapata lita 20 za mafuta, Afisa Kilimo wa Halmashauri hiyo, Zawadi Mwampashe amesema kuwa hekari moja inatakiwa iwe na skwea mita 4050, huku mstari hadi mstari iwe sentimita 75 na shimo hadi shimo sentimita 30 ambapo itakuwa na mimea isiopunga 18, 000 hadi 22,000.
Akiongelea kuhusu kiwango cha mafuta, Mwampashe amesema kuwa ukitumia mbegu bora zinao uwezo wa kutoa kila debe 6 zinaweza kuwa na kilo 73 ambapo zinauwezo wakutoa mafuta lita 23 nje ya makapi.
Kwa upande wake Mwanakikundi cha Amani toka Wilaya hiyo kinachojishughulisha na kilimo cha mbogamboga na usindikaji wa karanga, chili sauce, mbogamboga za kukausha, ubuyu, pilipili na jam, Flora Richard amesema kuwa wamejifunza aina ya mbegu bora kwa manufaa bora, huku akiahidi kuifikisha elimu hiyo katika kikundi chake na waliokuwa jirani zao.
“Tumepata maarifa na elimu ya uzalishaji bora wa mazao unaotolewa na Wataalam ili kuepukana na kilimo cha mazoea ili tulime kilimo cha kisasa kibiashara kinachoendana na uchumi wakati kwa wajasiriamali,” amesema Richard
Naye Mshindi wa zao la mahindi kanda ya Kati, toka Wilaya hiyo kata ya Kyengege Kijiji cha Mgundu,
Yesaya Njolle amesema kuwa wamejifunza kuwa kilimo kinauwezo wa kumtoa Mkulima katika umasikini na kwenda kwenye hali ya kati ya maisha.
Ameongeza kuwa kilimo cha kisasa kwa wakati wa masika na kile cha kiangazi ikiwa masharti yatafuatwa kwa kuzingatia maarifa na weledi walioupata wanaouwezo wakupata mazao msimu wa kipwa na masika.
MWISHO
Mkulima na mjasiriamali wa Kata ya Mtekente Wilayani Iramba Mkoa wa Singida aliyebuni Pawatila akilionesha katika siku ya sikukuu za Nane nane. Picha na Hemedi Munga
Afisa Kilimo wa Wilaya ya Iramba, Zawadi Mwampashe akiwafafanulia wakulima waliokuwa wakipata mafunzo ya nanma bora ya kulima katika viwanya vya Wilaya ya Iramba lililopo Jijini Dodoma katika siku ya sikukuu za Nane nane. Picha na Hemedi Munga
Wakulima waliofika katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Jijini Dodoma kwenye siku ya maonesho ya Nane nane. Picha na Hemedi Munga
Mtaalam toka kampuni ya Export Trade Group toka arusha linaloendesha upandaji wa mbegu mbora katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba lililopo Jijini Dodoma katika viwanja vya Nane nane mwaka huu, Abdul Abassy akionesha matunda yapatikanayo tokana na mbegu bora katika bustani. Picha na Hemedi Munga
Mwana kikundi cha Amani toka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Flora Richard akieleza namna alivyojifunza namna ya kulima kisasa kwa manufaa zaizi. Picha na Hemedi Munga
Mshindi wa kanda ya kati kwa zao la Mahindi toka Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Yesaya Njolle akieleza namna alivyojifunza namna ya kulima kisasa kwa manufaa zaizi. Picha na Hemedi Munga
Nanma mazao yalivyopendeza katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba vilivyoko Jijini Dodoma kwenye maonesho ya siku ya Nane nane.Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.