Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni amewaagiza Wamiliki wa Maduka ya Dawa na Maabara za Binaadamu kufuata kanuni, taratibu na miongozo mbalambali ya kutoa huduma hiyo muhimu kwa maisha ya mwanadamu.
Mwageni ameyasema hayo leo Jumamosi Januari 25, 2020 wakati akiongea na Wamiliki hao katika kikao kazi Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri hiyo mjni hapa.
“ Kila mmoja anapaswa kufahamu sheria inayomuongoza kufanya hizi shughuli na hukumu zake,” alisisitiza Mwageni na kuongeza
“ Mnafanya biashara zinazookoa uhai wa binaadamu hivyo mnapaswa kuchukua tahadhari mnapotoa huduma hizo”
Kuchukua tahadhari kunasababisha kuepusha madhara yanayotokana na Wamiliki ambao hawafuati taratibu na kanuni ya kuendesha maduka hayo.
“Ninawaagiza Wamiliki wote wa Maduka ya Dawa na Maabara za Binaadamu kuingia kwenye shughuli hii ili kuisaidia wilaya kutoa huduma zinazostahiki na si kutoa huduma ili kukuza mtaji,” amesema Mwageni
Vilevile amewatahadharisha Wamiliki hao kuchukua dawa serikalini kuwa ni rahisi kufahamika na nisababu yakufirisika.
Awali akiwasilisha taarifa ya Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Kaimu Mganga Mkuu Afisa Ustawi wa Jamii, Hapiness Alex amesema duka la dawa muhimu ni miongoni mwa biashara zinazodhibitiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa sheria ya Baraza la Famasi.
Wilaya hiyo inajumla ya maduka ya dawa muhimu 121 na maabara 11 katika vijiji, mitaa na vitongoji mbalimbali.
Pia amemuahidi Mkurugenzi huyo kuendeleza usimamizi shirikishi unaolenga kufuatilia huduma zinazotolewa na maduka ya dawa muhimu, uhai wa vibali vya maduka hayo na utendaji kazi na uhai wa vibali vya maabara za binaadamu.
Tabia hiyo husaidia kujenga uhusiano mzuri na kuimarisha huduma za afya katika vijiji, mitaa na vitongoji vyote.
Naye ndugu Joseph wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ameawataka wamiliki hao kutunza nyaraka za manunuzi kutokana na uwepo wa dawa ambazo hazina usajili na si salama, hivyo itaturahisishia kuzifahamu wakati wa ukaguzi na kuwachukulia hatua wanaohusika.
“Ninawaagiza kununua dawa zilizoandikwa majina ya dawa na majina ya kampuni yaliozalisha dawa hizo,” amesema
Akiongea katika kikao hicho Afisa Biashara wa Wilaya hiyo, Prosper Banzi amewataka Wamiliki hao kufuata utaratibu wa kupata leseni na kusoma vizuri masharti yake.
“ Ni bora tuwe na wafanya biashara wachache wanaofuata kanuni, vigezo na masharti ambayo mmewekewa na sekta zote,” amesema
Pia amewaambia kuwa ukaguzi wa leseni unaendelea na hivyo atakayebainika kukiuka sheria ya leseni atapigwa faini.
Akichangia mada mmoja wa Wamiliki wa Maduka kwa niaba ya wengine, Alex Paneras ameuomba uogozi kuwapa ushirikiano mzuri pindi wanapokuja kukagua maana mara nyingi huwa wanawafikiria kuwa ni vibaka kutokana na tabia na muonekano wao na kuwataka Wamiliki wenzake kuwa makini.
Afisa Ustawi wa Jamii, Hapiness Alex akiwasilisha taarifa ya Mganga Mkuu inayohusu Wamiliki wa Maduka ya dawa na Maabara za Binaadamu mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo. Picha na Hemedi Munga
Wamiliki wa Maduka ya dawa na maabara za Binaadamu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika kikao hicho. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.