Na Hemedi Munga
tehama@irambadc.go.tz
Singida - Iramba. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoni Singida, Mhandisi Michael Matomora amesikiliza na kutatua changamoto ya kulipa kodi ya vibanda iliyodaiwa kuwa kubwa na wafanyabiashara wa mji mdogo Kiomboi.
Matomora ametatua changamoto hiyo mwishoni mwa juma hili alipokutana na wafanyabiashara hao katika ukumbi Mkubwa wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Akiongea katika kikao hicho Mkurugenzi huyo, amewataka wafanyabiashara hao kulipa kodi ili Halmashauri iweze kukusanya mapato na kufikisha miundombinu mbalimbali katika soko na stendi.
“Ndugu zangu wafanyabiashara ni lazima tufahamu kuwa kulipa kodi ni lazima, hivyo nilazima tukubaliane kodi ya kizalendo ambayo kila mmoja kuanzaia leo baada ya kikao hichi atakwenda kulipia kodi ya kibanda anachomiliki kilichopo katika eneo la Serikali.” Alisema Matomora na kuongeza kuwa
“Siwezi kukubali kuwa na soko chafu kiasi hicho, hivyo tumeanza kuweka umeme na miundombinu mingine itafuata mpaka pawe pazuri na rafiki pakufanyia biashara muda wote.”
Katika kikao hicho wamakubaliana kila mwenye kibanda kulipia kiasi cha Tsh 10000 kila mwisho ya mwezi ukilinganisha na Tsh 20000 iliyokuwa ikilipwa kabla ya kikao hicho.
“Mimi naridhia kuanzia Februari mosi, 2022 mkalipie Tsh 10000 kila tarehe ya mwisho wa mwezi, hivyo vibanda vyote wamiliki wake waende wakalipe kodi kwa sababu sitaki kusikia mfanyabiashara anatengeneza deni sinta weza mvumilia.” Alisistiza
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kwenda kulipa madeni amabayo wamekwisha yatengeneza katika mfumo wa mapato kwa kuwa hakuna namna wa kuyafuta madeni hayo ispokuwa ni kwa kulipa madeni.
Alifafanua kuwa kiwango cha Tsh 10000 ni kiwango kidogo ambacho mfanyabiashara anaweza kulipa kodi hiyo huku akiweka utaratibu mzuri wa kulipa deni.
Awali akiongea katika kikao hicho Afisa Biashara wa Halmashauri hiyo, Prosper Banzi aliwapongeza wafanyabiashara hao kwa sababu wamekuwa na subira dhidi ya mgogoro huo uliodaiwa kuwapo kwa muda mrefu.
“Hongereni sana kwa uvumilivu, hali hii inatujengea taswira mpya ya kulitekeleza jukumu la kulipa kodi ya vibanda kwa wakati kwa sababu sasa ni kodi ambayo mmeipanga wenyewe.” Alisema Banzi
Kwa upande wake mmoja wa wafanyabiashara hao, Omari Haruna alishukuru kwa kiwango cha Tsh 10000 na kuahidi kuwa maamuzi hayo yaliofikiwa katika kikao hicho itakuwa ni sababu ya kuendelea kurekebisha vibanda vingine ili Halmashauri ipate mapato mengi.
“Kwa kweli wastani wa kodi hii ninauhakika wafanyabiashara hawa watalipia na kuendeleza vibanda ambavyo vilikuwa ni magofu kutengenezwa kuwa safi na tayari kwa kuvilipia kodi.” Alisema Haruna
Naye mmoja wa wamiliki wa vibanda vya sokoni, Winjuka Msangulo alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa makubaliano ambayo wameyafikia na kuahidi kuwa sasa watakuwa tayari kulipia kodi hiyo.
Aidha alisema kuwa watakuwa ni mabalozi watakofikisha ujumbe wa kulipia kodi ya vibanda kwa wamiliki wote ambao hawakufanikwa kufika katika kiako hicho.
“Nikuombe Mkurugenzi kwa wafanyakazi wako kuwa makini pale mteja anapokuja lipia deni lake apate bili iliokuwa sahihi kulingana na deni lake.” Aliomba
MWISHO
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.