Walimu wakuu kwa kushirikiana na walimu wao wa michezo wa shule za sekondari zipatazo23 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, wamepokea vifaa mbali mbali vya michezo kutoka katika kampuni ya vinywaji baridi nchini Coca cola.
Zoezi hilo limeweza kufanyika katika ukumbi mdogo wa mikutano uliopo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na kuhudhuriwa na walimu wakuu na wengine kuwakilishwa na walimu wao wa michezo, nakupokea jezi 36 za mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwagenia ameshukuru kampuni ya Coca-Cola kwa kutoa zawadi hizi za michezo. Ameongeza kusema zawadi hizo zitafanikisha jitihada za kuendelea kuibua vipaji vya wachezaji chipukizi wa michezo ya soka mpira na kikapu. alisisitiza kuwa sekta ya michezo inazidi kukua ambapo hivi sasa lengo lake sio burudani bali ni biashara kubwa.
Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kampuni ya Coca cola Mkoa wa Singida Ndg. Benjamin Daud ambaye ameudhuria katika ufanyikaji wa zoezi hilo Wilayani hapa, amesema kwamba zoezi hili hufanyika kila mwaka kwa ushirikiano wa Maafisa Elimu Michezo na Utamaduni katika wilaya hii. Aliongeza kusema kampuni ya Coca-Cola inajivunia kuhamasisha michezo katika Wilaya ya Iramba kwa kutoa vifaa vyamichezo katika shule 23 za sekondari. “naamini vipaji vingi vinaibuliwa na vitaendelea kuibuliwa baada ya kutoa vifaa vya michezo” alisema Ndg. Benjamin.
Ndg.Benjamin alisema kwamba wameweza kugawa kwa kila shule za elimu sekondari wilayani Iramba Jezi za mpira wa Miguu 18 na mpira wa Kikapu 18 jumla yake 36 pamoja na Mpira wa miguu mmoja na wa kikapu mmoja kwa kila shule za sekondari zipatazo 23 Wilayani hapa.
Lengo haswa la ugawaji wa vifaa vya michezo kwa shule hizo za sekondari Ndg. Benjamin ameeleza kwamba ni kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi mbali mbali katika shule hizo za sekondari pamoja na kampuni hiyo kuweza kuwa karibu na jamii.
Nao walimu wa shule hizo za sekondari waliweza kuishukuru kampuni hiyo ya vinywaji vya Coca cola kwa kusema kwamba, imesaidia kukuza vipaji vya wanafunzi wao pamoja na mazingira ya wanafunzi hao kupenda zaidi masomo.
Vifaa hivyo vya michezo kwa wanafunzi wa shule za sekondari hutumika katika mashindano mbali mbali yakiwemo mashindano ya UMISETA pamoja na Copa Coca cola.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwakilishi wa Kampuni ya Coca cola Mkoa wa Singida Ndg. Benjamin Daud, Walimu wakuu na walimu wa michezo wa shule za sekondari baada ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu za sekondari Wilayani Iramba mkoa wa Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.