Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Singida Mhe. James J. Mkwega ameongoza kikao hicho wilayani Iramba na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo msimu wa kilimo, mikakati ya kupokea wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2018/2019, utoaji wa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo wadogo na kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyopo halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Akizungumza kwenye mkutano wa ALAT Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula ambaye ni Mgeni rasmi, amepongeza mkutano wa ALAT kwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutatua changamoto zilizopo kwenye halmashauri zetu. “Nawapongeza sana wajumbe wa ALAT kwa kazi nzuri mnazozifanya katika kusimamia serikali za mitaa. Natambua juhudi zenu nzuri jinsi mnavyoshiriki kuleta maendeleo katika maeneo yetu kwa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo, endeleeni na utaratibu huu wa kufanya ziara za mara kwa mara za kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa”. alisema Mhe. Luhahula
Alisisitiza wajumbe wa ALAT kusimamia kilimo cha mazao ya Alizeti, Pamba na Korosho, katika ngazi ya kijiji na kata ili yawe mazao ya kudumu ya biashara kwa wananchi wa mkoa wa singida. “Mazao yetu ya kimkakati katika mkoa wetu ni Alizeti, Pamba na Korosho. Viwanda tulivonavyo katika mkoa wetu wa singida vinauwezo wa kukamua mbegu za Alizeti tani laki 482, tunazalisha tani laki 260 tu, tuna upungufu mkubwa sana, lazima wananchi walime Alizeti kwa kutumia mbegu tija kwa utaratibu na kanuni bora za kilimo ili kuhakikisha tunapata tani 482. Tukiboresha mazao haya ya kimkakati, tukawa na Pamba, Korosho na Alizeti tutatengeneza mfumo mzuri wa kununua kupitia kwenye ushirika, Halmashauri zetu zitapata ushuru wa kutosha na vyanzo vyetu vitakuwa vimeongezeka”. Alisisitiza Mhe. Luhahula
Aidha Mhe. Luhahula amezitaka halmashauri ziendelee na ubunifu wa kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuinua kiwango cha ukusanyaji wa mapato katika ngazi ya halmashauri na vyanzo vya mapato viimarishwe na kusimamiwa.
Vile vile Mhe. Luhahula amesisitiza kuhakikisha wananchi wanafanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli ya kuipeleka nchi kwenye uchumi wa kati na viwanda. “ALAT hamuwezi kujitenga na serikali kuu katika kutekeleza na kuleta uchumi ambao serikali yetu inataka tufike. Tumeona kazi kubwa ambazo Mhe. Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli anazozifanya kutengeneza viwanda vipya zaidi ya 3066, ujenzi wa Miundombinu ya Barabara na madaraja, Ujenzi wa reli ya mwendo kasi ya stanadard gauge, Ujenzi wa mradi wa umeme wa stieglers gorge, Ununuzi wa ndege 7, Ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya na hosipitali, Ujenzi na ukarabati wa nyumba za wakuu wa wilaya na Watumishi, ujenzi na ukarabati wa vyuo, shule za sekondari na msingi, Elimu bila malipo na miradi mingine mingi alisema Mhe. Luhahula
Aliongeza kusema, kila mmoja wetu atambue na atimize wajibu wake ili tuhakikishe tunawasaidia wananchi wetu. “tukawasaidie, tukawasemee, wananchi wetu wakati mwingine wanateswa na Rushwa, Waheshimiwa madiwani ni watu ambao mna nafasi ambazo mnaweza kusimama na kutetea wananchi wenu mahala walipo, ukisimama wewe kidedea mwananchi hawezi kuonewa kule. Lazima uchumi wa kati umufikie mwananchi. Alisisitiza Mhe. Luhahula.
Wajumbe wa ALAT wakifuatilia majadiliano katika kikao hicho yakiendelea katika wa halmashauri ya wilaya ya Iramba katika ukumbi wa halmashauri.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.