Mkuu wa Mkoa Singida Mhe. Peter Serukamba amezindua miradi mitatu ya Maji kwenye vijiji vya Kaselya, Zinziligi na Maluga yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 1.4 Iliyopo Wilayani Iramba.
Akiongea baada ya kuzindua mradi huo RC Serukamba amempongeza Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya lramba Mhandisi Ezra Mwacha na watendaji wake wote kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuhakikisha mradi huo uliogharimu shilingi bilioni 1.4 unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa na kupelekea kuimarisha huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo.
Aidha, ameielekeza RUWASA kuhakikisha huduma ya maunganisho ya maji inatolewa kwa wananchi bila vikwazo na kuhakikisha zoezi la usomaji wa dira za maji unafanyika kwa ufanisi na kwa kuwashirikisha wananchi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya lramba Suleiman Yusuph Mwenda ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizowezesha kukamilika kwa miradi huu na kuleta neema ya majisafi.
Katika Hafla hiyo ya uzinduzi wa miradi hiyo ya maji katika vijiji vya Kaselya,Zinziligi na Maluga viongozi mbalimbali wa Chama na serikali waliohudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya lramba Ndugu Samweli Asher Joel, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya lramba Mhe. Innocent Msengi na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya lramba wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Marietha Kasongo
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.