Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi afanya ziara ya uzinduzi wa mradi wa Maji katika Kijiji cha Ng’anguli Kata ya Maluga Tarafa ya Kinampanda Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida
Mradi wa Maji katika kijiji cha Nganguli unahusisha Tank moja la kuifadhi maji lenye ujazo wa M350, Kisima kimoja na Mashine,DP au vituo vya kuchotea maji 11, milambo 2 ya kunyweshea mifugo na Mtandao waMabomba wenye urefu wa km.9.5, visima 3 vya pamou za Mkono,
Mradi huu unazalisha zaidi ya lita 3050000 kwa mwezi na unahudumia vitongoji vitatu vya Ng’anguli, Ikyeto na Masunkune vyenye jumla ya Kaya 586 zenye watu 3332 na Mifugo kwa Mchanganuo ufuatao: Ngombe 5575, Punda 68, Mbuzi 1,303 na Kondoo 627. Aidha Mradi unahudumia baadhi ya Vitongoji katika vijiji jirani vya Makunda, Misuna, na Tumli.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa na Mkuu wa Wilaya wa Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Iramba Bwana. Linno Mwageni na Uongozi kutoka Mkoani Singida na Viongozi Kutoka Halmashauri ya Iramba wakiwa kwenye Picha ya Pamoja kwenye ziara ya uzinduzi wa mradi wa Maji Kijiji cha Ng’anguli Kata ya Maluga Tarafa ya Kinampanda Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.