Meneja wa shirika la World Vision kanda ya kati Ndg. Faraja Kulanga akikabidhi mabati 773 yenye thamani ya Tshs 18,126,500/= kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Picha kionesha zahanati ya Doromoni iliyoezuliwa paa kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha uharibifu wa vifaa tiba, dawa pamoja na jengo hasa paa zaidi ya robo tatu imeezuliwa na upepo mkali ambapo mbao, ceiling bodi, bati na madirisha vyote vimeharibika sana na upepo huo.
vyumba vitatu (3) vya madarasa ya shule ya msingi Doromoni vilivyoezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali kijiji cha Doromoni kata ya Tulya wilayani Iramba.
Picha ikionesha baadhi nyumba za wananchi wa kijiji cha Doromoni zilizoezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali katika kijiji cha Doromoni kata ya Tulya wilayani Iramba.
Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula akiongea na wananchi wa kijiji cha Doromoni kata ya Tulya kwenye ziara ya Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kutembelea wananchi waliopatwa na maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mhe: Simion Tyosera akiongea na wananchi wa kijiji cha Doromoni kata ya Tulya kwenye ziara Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kutembelea wananchi waliopatwa na maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni akiongea na wananchi wa kijiji cha Doromoni kata ya Tulya kwenye ziara Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kutembelea wananchi waliopatwa na maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali.
Mwakilishi wa Prof. Kitila Mkumbo wakili Jacob Lyanga akikabidhi risiti ya ununuzi wa mifuko 100 ya saruji kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameafanya ziara ya kutembelea wananchi waliopatwa wa maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kijiji cha Doromoni kata ya Tulya tarafa ya kisiriri wilayani Iramba mnamo tarehe 09/04/2019 siku ya jumanne.
Kijiji cha Doromoni kilichopo kata ya Tulya kilikumbwa mvua iliyoambatana na upepo mkali ambapo vyumba vitatu (3) vya madarasa ya shule ya msingi Doromoni viliezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali, zahanati ya Doromoni pia iliezuliwa paa kutokana na mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha uharibifu wa vifaa tiba, dawa pamoja na jengo hasa paa zaidi ya robo tatu imeezuliwa na upepo mkali ambapo mbao, ceiling bodi, bati na madirisha vyote vimeharibika sana na upepo huo, sambamba na nyumba 39 za wananchi wa kijiji cha Doromoni ikiwa pamoja na uharibifu wa mali zao kama mazao shambani na mifugo.
Akizungumza na wananchi wa Tulya, Dkt. Nchimbi amewashukuru sana Wadau waliojitokeza kutoa msaada kwa wananchi waliopatwa wa maafa hayo amesema “Lengo kubwa la kuja hapa ni kuwapa pole na kupokea misaada mbalimbali ambayo imetolewa na Wadau wetu na kukabidhi misaada hii kwa wananchi waliopatwa na maafa, nawashukuru sana misaada hiyo imelenga pia wananchi mmoja moja, ili kuboresha nyumba zao, ndugu zangu majanga yanapotokea kama maafa haya yanakuja na sura nyingi, kuna maafa hayazuiliki, kwa hiyo tunajikuta tuko kwenye hali kama hii kutokana na yaliyotokea. Baada ya maafa haya mliungana na kuona jinsi ya kukabiliana na maafa haya ndo maana Wadau wetu wamejitokeza kutoa misaada kwa wananchi, huu ni msaada mkubwa sana kwa wananchi. Tuendelee kuwa wamoja. Tunapofikiri kurudisha majengo yetu, lazima tujenge nyumba ambazo ni bora zaidi ili kukabiliana na majanga haya alisema Dkt. Nchimbi.
Watendaji wote wa kata, vijiji wapewe Elimu kuhusu nini kinachofanyika kwenye ujenzi ili wazungukie wananchi na kutoa ushauri wa msingi kwenye masuala mazima ya ujenzi na ikibidi waweze kuzuia pale ambapo watabaini mapungufu kwenye ujenzi na wananchi wote lazima kupokea ushauri ili kuepukana na maafa haya alisisitiza Dkt. Nchimbi
Adiha Dkt. Nchimbi ameongeza kusema “Ziwa Kitangiri lisitazamwe kwa mazoea kwababu ya tabia nchi, mahali hapa ni eneo la bonde la ufa, wataalamu naomba mtoe Elimu kuhusu tabia ya bonde la ufa. Ndo maana upepo ulikuwa mkubwa sana ili wananchi wajue ujenzi wa majengo yao. Kama itakuwepo ulazima wa mwananchi kuhama ili kuepukana na maafa yanayoweza kutokana na ziwa lazima mfanye hivyo ili kuchukua taadhali”.
Wadau waliochagia shirika la World Vision bati 773, Sekenke one bati 200, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba mifuko ya saruji 150, Prof. Kitila Mkumbo mifuko ya saruji 100, Hamad S. Adimu Tshs100,000/=, Mohamed S. Adimu Tshs100,000/=, Abdala S. Adimu Tshs100,000/=, Jabili Ahamed Tshs50,000/=, Edward Makundi Tshs50,000/=, Ally Said Tshs20,000/=, Ally Msangi Tshs50,000/=, Joseph Mhindi Tshs50,000, Waziri Hussein Tshs500,000. Michango iliyopokelewa Jumla kuu bati 973, Mifuko ya saruji 250 na Fedha taslimu Tshs1,220,000/=
Dkt. Nchimbi amesistiza “wajasiliamali lazima wawe na Vitambulisho, kufanya hivyo tutakua tunaunga mkono juhudi za Mhe: Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, wajasiliamali wasisumbuliwe, wasitozwe ushuru wowote, wachangie elfu 20,000/= ambayo ni gharama ya kutengeneza kitambulisho hicho,
Ameongeza kusema “Kuna wakulima wa mazao mbalimbali, sote tunaona hali ya hewa, hakikisheni wananchi mnatunza chakula, mwenye mfugo avune na kununua chakula maana ni fedhea sana familia kukosa chakula Wananchi lazima mtunze chakula, lakini wewe mkulima unayesafirisha mazao yako kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ukibeba tani moja au chini ya tani moja hautotozwa ushuru wowote , unasafirisha bure, hakuna atakayekusumbua lakini kuna watu ambao wanajifanya wakulima lakini sio wakulima, ni wafanyabiashara na madalali, wafanya biashara lazima walipe ushuru alisisitiza Dkt. Nchimbi
Dkt. Nchimbi amesema “Maagizo na maelekezo ya Mhe: Rais, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, yametimia katika mkoa wetu wa Singida kuwa kila mkoa kufungua kituo cha kuuzia dhahabu, tiyaari mkoa wa Singida tunacho icho kituo, dhahabu zetu sasa zitakuwa zinauziwa hapa mkoani kwenye jengo la serikali la Ofisi za madini ili kuwasaidia wachimbaji kuuza dhahabu yao kwa bei halisi na kudhibiti walanguzi katika maeneo ya wachimbaji pia tumefungua vituo vya kukusanyia Dhahabu shelui na sekenke ili kudhibiti wizi na uuzwaji holela wa madini ya dhahabu katika maeneo hayo. amesema Dkt. Nchimbi.
Ameongeza kusema wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakiksiha watoto wao wanapata elimu, “wazazi hakikisha mnapeleka chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu na hatimaye waweze kufaulu mitihani ya Darasa la saba”.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.