Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt, Rehema Nchimbi, amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kinampanda kilichopo kijiji cha Kyalusangi Wilayaya Iramba,
Dkt Nchimbi, amewaasa Wananchi wa eneo hilo kuendeleza ushirikiano kwa pamoja katika kuhakikisha ujenzi wa majengo hayo katika kituo cha afya Kinampanda yanakamilika katika muda sahihi iliyaweze kuanza kutumika kutolea huduma za Afya kwa wananchi.
Amewataka viongozi wa nyazifa mbali mbali wakiwemo, Diwani, Watendaji na Wenyekiti wa vijiji na vitongoji, kuwahamasisha wananchi wao kwa nguvu ya pamoja ilikuhakikisha wanashirikiana katika zoezi hili la ujenzi wa kituo cha afya cha Kinampanda.
Dkt, Nchimbi amesema kwamba, ucheleweshwaji wa ujenzi katika majengo hayo kutakwamisha mambo mengi muhimu katika huduma za afya ikiwemo huduma hiyo kuchelewa kuwafikia wananchi.
Diwani wa Kata ya Kinampanda(CCM), Mhe. Justus Makala amewaasa wananchi wake kutoa michango ya elfu Thelathini kwa kila Kaya ili kumalizia kazi ya ujenzi katika kituo hicho cha Afya.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi ameweza kuchangia Shilingi Laki mbili kuunga mkono wananchi wa Kinampanda kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya hicho.
Mkuu wa mkoa Dkt, Rehema Nchimbi akiongea na wananchi wa Kyalosangi kwenye ziara ya kukagua Maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kinampanda.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.