Hemedi Munga, Irambadc
Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa kuwa ya kwanza na kutoa mshindi wa kwanza kanda ya kati kwa zao la Mahindi katika kilele cha Maonesho ya Nane Nane mwaka huu.
Dkt. Nchimbi ametoa pongezi hizo wakati alipokuwa akiongea na wakulima na wajasiriamali waliohudhuria maonesho hayo katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki hii.
Akiongea katika hafla hiyo, Dkt. Nchimbi amesema kuwa kuja kwa maonesho ya Nane Nane Jijini Dodoma kumeleta nuru kwa watu wanaoishi katika jiji hilo.
Pia ameonesha kuwa kanda ya kati ni tajiri kwa kuwa lina madini ya dhahabu na yureniam.
“Tumeombe Mungu na sisi tupate bonge kubwa la dhahabu, inaweza tokea, hivyo kuendelea kuimarisha utajiri wa kanda ya kati na kuifanya kuwa kama ulaya,” amesema Dkt. Nchimbi na kuongeza kuwa
Akiongelea kuhusu kauli mbiu ya Nane Nane mwaka huu isemayo “kwa maendeleo ya kilimo na uvuvi chagua kiongozi bora, Dkt. Nchimbi amesema kuwa kilicho bora huzaa bora, hivyo kilichotufikisha hapa ni uongozi bora na tuna haki ya kumshukuru Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Halikadhalika Dkt. Nchimbi amewata wataalam walio onesha teknolojia ya magari na mitambo wezeshi kufika katika halmashauri zote za kanda ya kati kwa lengo la kutoa elimu ili teknolojia hiyo iweze kutumiwa na Halmashauri hizo.
“Teknolojia hiyo ni rahisi na garama yake pia ni rahisi, hivyo wakulima wengi wataweza kuitumia kwa urahisi ili wapate mavuno mengi” amesisitiza Dkt. Nchimbi
Pia amewataka wahusika hao kuhakikisha wanafikisha mbegu bora za mifugo katika halmashauri zote na kuwaasa wafygaji kuwa na mifugo michahche yenye ubora badala ya kuwa na mifugo mingi isiokuwa na ubora.
Pia amegiza kila Halmashauri kuwa na shamba la malisho huku akiahidi kuwa Nane Nane kutakuwa na tuzo ya malisho bora.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Jene Ng’ondi amewashukuru wajasiriamali na wakulima wote kwa kuwezesha Halmashauri hiyo kupata ushindi wa Mkulima bora wa zao la Mahindi kwa kanda ya kati na kuifanya Halmashuri hiyo kuwa ya kwanza kati ya Halmashauri saba za Mkoa wa Singida katika maonesho hayo.
Aidha amewata wakulima hao kuanza maandalizi mapema ya Nane Nane ijayo kwa kuwa mwisho wa Nane Nane hii ndio mwanzo wa Nane Nane ya mwaka ujao.
Naye mmoja wa wakulima kwa niaba ya Wajasiriamali na Wakulima hao Mgundu,
Yesaya Njolle amesema kuwa wamejifunza kuwa kilimo kinauwezo wa kumtoa Mkulima katika umasikini na kwenda kwenye hali ya kati ya maisha.
Ameongeza kuwa kilimo cha kisasa kwa wakati wa masika na kile cha kiangazi ikiwa masharti yatafuatwa kwa kuzingatia maarifa na weledi walioupata wanaouwezo wakupata mazao msimu wa kipwa na masika.
MWISHO
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Jene ng’ondi akiwa na Mshindi wa Kanda ya Kati kwa zao la Mahindi, Yesaya Njolle
pamoja na Wajasiriamali na wakulimwa wengine waliokuwa wakimpongeza katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma katika kilele cha Siku ya Nane Nane. Picha na Hemedi Munga
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Jene ng’ondi akiwa na Mshindi wa Kanda ya Kati kwa zao la Mahindi, Yesaya Njolle katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma siku ya kilele cha Nane Nane. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.