Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewaapisha Wazee Wapya wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Iramba ambapo watahudumia kwa kipindi cha miaka mitatu.
Tukio la kuwaapisha Wazee hao limefanyika leo Alhamisi Januari 16, 2020 katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya hiyo.
Wazee wa nne wa Baraza hilo ambao wameapishwa leo ni Agness Mbazi, Ainess Shimba, Omari Hassan na Fanuel Kiula kuchukuwa nafasi ya Paulo Sankey, Joram Masenga na Elimamba Lula ambao wamemaliza muda wao.
Dkt, Nchimbi amewaambia Wazee hao kuwa thamani ya kiapo chao ni kudhihirisha matunda na matokeo ya utumishi wao kwa wananchi.
Huku akiwataka kuthamini ardhi kwani kufanya mambo kinyume na maadili ardhini sio tu kunaikosea ardhi ispokuwa ni kulifanyia kosa Taifa kwa kuwa linajengwa na Ardhi.
“Tanzania bila ardhi haiwezi kuwepo, Mataifa makubwa ni Ardhi,” alisisitiza Dkt Nchimbi
Mkuu huyo amefafanuwa kuwa ardhi ni uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa ambapo Tanzania ya viwanda haiwezi kuwepo pasipo ardhi.
Aidha amewaomba Wazee hao kutumia muda mwingi kutoa elimu kwa watendaji wa kata, walimu wa shule wanazoweza kuzifikia na wananchi kwa ujumla ili kujenga uwelewa wa pamoja.
“Mwiba hutokea ulipoingilia, nanyi Baraza la Ardhi mkikaa salama mtatatuwa migogoro ya ardhi kwa kuwa mnajuwa namna ilivyoanza,” amesema Dkt, Nchimbi
Pia amewataka kuepuka rushwa na kupindisha haki wakati wakiwahudumia wananchi huku akiwahimiza kuwa mfano wa kuingwa , kujifunzia nakuwa namba moja kimkoa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Angelina Lutambi amewataka Wazee hao kufahamu kuwa kuna migogoro mingi wanayopaswa kuitatuwa kwa hekima zao.
“ Mlipo apishwa mmekabidhiwa jukumu zito na nikiwatazama ninawaona mmejaa hekima,” amesema Dkt, Lutambi
Amewafafanulia kuwa mwananchi anapofika kwao anamatumaini kupata haki kwa kutumia miiko ya katiba, sheria na vigezo vinavyotumika kwa uwadilifu.
“ Tunaweka imani kwenu kuwa maamuzi mtakayoyatoa katika Baraza la Ardhi hayata iletea serikali picha mbaya wala mabango pindi viongozi wakitaifa watakapotembelea wilayani Iramba,” amesisitiza Lutambi
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewataka Wazee hao kutambuwa kuwa wanalojukumu la kuhudumia wilaya ya Iramba na Mkalama.
Pia amewaagiza kutenda haki pindi watakapokuwa wakiwahudumia wananchi .
“ Haki huinuwa Taifa, mtakapo haribu haki, mtasababisha wananchi kuichukia serikali,” amesema Luhahula
Awali Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi wa Halmashauri hiyo , Baraka Shuma amesema Wazee wa Baraza ni kiungo muhimu na nisehemu ya Baraza.
“Baraza limekamilika na sasa tupo tayari kuwahudumia wanachi,” amesema Shuma
Waliohudhuria tukio hilo la kuapishwa Wazee wa Baraza wameonesha kuwa na imani na Baraza hilo kwa kuwa lina kiongozi wa dini ambaye ni mjumbe katika Baraza.
Wazee Wapya wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Iramba ambao wameapishwa leo Alhamisi 16, 2020 na Dkt, Rehema Nchimbi Mkuu wa Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Mmoja wa Wazee Wapya wa Baraza la Ardhi na Nyumba wilaya ya Iramba akiapa mbele ya Dkt, Rehema Nchimbi Mkuu wa Mkoa wa Singida. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Baraza la Ardhi walioapishwa jeo Alhamisi Januari 16, 2020 kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula na Kulia kwa Dkt, Nchimbi ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Baraza la Ardhi walioapishwa jeo Alhamisi Januari 16, 2020 pamoja na viongozi malimbali wa dini. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na Wazee wa Baraza la Ardhi walioapishwa jeo Alhamisi Januari 16, 2020 pamoja na waku wa Idara Mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.