Hemedi Munga, IrambaDC
Iramba – Singida. Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi ameukabidhi Mwenge wa Uhuru 2019, kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwandri leo Agosti 26, 2019 Mgongoro mpakani mwa Singida na Tabora.
Akikabidhi Mwenge huo, Dkt. Nchimbi amemueleza Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuwa mwenge wa Uhuru, unawaka, unameremeta, na kwa heshima zote za kumuwakilisha Rais Jonh Pombe Magufuli pamoja na itifaki yote ya mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 ipo salama.
Akitoa taarifa fupi ya mbio za Mwenge wa Uhuru, Dkt. Nchimbi amesema kuwa Mwenge wa Uhuru umekimbizwa kwa siku saba sawa na kilometa 804.8 katika Halmashauri saba za mkoa wa Singida huku ukiwa umepitia jumla ya miradi 46.
Miradi ambayo inahusu sekta ya elimu, afya, mazingira, maji, utawala bora, kilimo, ushirika, biashara, elimu ya mpiga kura, program za mapambano dhidi ya dawa za kulevya, malaria, rushwa na UkIMWI. Aliongeza Nchimbi
Akieleza suluhisho la vijana walio maliza JKT wa oparesheni Magufuli, oparesheni Kikwete na oparesheni nyinginezo Mkoani Singida amewataka vijana kuchukua mizinga ili wafuge nyuki wajipatie kipato kizuri na waachane na ukataji wa miti unaoharibu mazingira.
Ameyasema hayo mbele ya mkimbiza mwenge kitafa, Ndugu Mzee Ali ukiwa ni mkakati wa pili unaoitwa achia shoka kamata mzinga ulioanzishwa mkoani Singida kwa lengo la kuachana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa kutafuta kipato.
“Tumesema waachie shoka wakamate mzinga, ukiwa na mizinga ukifuga nyuki, unatunza mazingira ambayo ni vyanzo vya maji.” Alisema nchimbi
Mkakati wapili unakuja baada ya kufanikwa kwa mkakati wakwanza uliotabulika kama mshahara wangu uko wapi wenye lengo la kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanaona mishahara yao na kumpenda muajiri wao.
Mkakati huo ulizinduliwa na mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2018 na watumishi wameweza kuonesha mishahara yao kupitia kilimo,ufugaji, ufundi, uvuvi, ujasiriamali na mambo mengine na kuweza kuwa na miradi inayowawezesha kuwaajiri wengine.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwandri amekiri kuupokea Mwenge wa Uhuru 2019 na kuahidi kuulinda Mwenge wa Uhuru pamoja na wakimbiza mwenge kitafa kwa siku zote watakazokuwa Mkoani Tabora.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.