Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe : Dkt Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kukagua shughuli za uvunaji na uuzaji wa zao la pamba kwenye vijjiji vya mtoa, msai kata ya mtoa tarafa ya Ndago wilayani Iramba leo tarehe 20/06/2019.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe: Dkt Rehema Nchimbi aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno Mwageni, Viongozi wa Mkoa wa Singida na Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wamefanya ziara hiyo katika vijiji vya Msai na Mtoa.
Akizungunza na wananchi wa kata ya Mtoa Dkt Nchimbi amesema nimekuja kujionea zoezi la uvunaji na uuzaji, kama linaenda vizuri na pamba yote inayopokelewa na vyama vya Ushirika ni ile iliyo katika ubora unaohitajika.
Vile vile Dkt Nchimbi ameagiza uongozi kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la malipo kwa wakulima na kuhakikisha kwamba wanaouza pamba wote wanalipwa hapo hapo na ni marufuku mnunuzi kumkopa mkulima.
Pamoja na wingi huu wa pamba ambao tumezalisha katika wilaya yetu ya Iramba na katika mkoa wetu wa Singida, faraja kubwa tuliyonayo mnunuzi tuliyenaye amesema atanunua pamba yote kilo ni Tshs 1200, Viongozi wote lazima muwe macho na yeyote ambaye atajitokeza kudanganya wakulima lazima kupambana nae, mnunuzi wa pamba ni BioSustain.
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe: Dkt Rehema Nchimbi amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanatumia vizuri fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya zao la pamba.
Ameongeza kusema ni vema wakatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiletea maendeleo katika familia zao, kununua chakula, kuwapatia mahitaji muhimu watoto wao ili kuwaendeleza kielimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba bora na za kisasa.
Wakulima ambao walizungumza kwa nyakati tofauti, walitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuhamasisha wananchi walime zao la pamba, na kuwagawia pembejeo bure bila gharama yeyote na sasa wameanza kuona mafanikio.
Dkt Nchimbi amewashauri wakulima wa pamba baada ya kuuza pamba fedha zao zilipwe kupitia akaunti za benki au kwa kutumia M-pesa, Airtel Money n.k ili kuwa na usalama wa fedha zao. Aliongeza kusema wakulima walipwe kwa wakati na kwa kuzingatia sheria za ununuzi wa pamba pamoja na usafi na ubora wa pamba. Dkt Nchimbi alisema usafi na ubora wa pamba ni suala ambalo linapewa kipaumbele kikubwa kwa sababu uchafu kwenye pamba unaathiri ubora na sifa ya pamba katika soko la dunia.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.