Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt Rehema Nchimbi ameongoza maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika yaliyofanyika kijiji cha Doromoni kata ya Tulya Tarafa ya Kisiriri wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida leo tarehe 16/06/2018.
Dkt Rehema Nchimbi ameungana na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula, Mkurugenzi mtendajiwa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl Linno Mwageni, viongozi wa mkoa wa Singida, viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba na wananchi kuadhimisha siku ya mtoto Afrika.
Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi warangi. Watoto hao walikuwa wakidai haki zao za kutobaguliwa pamoja na haki nyingine za kibinadamu ikiwemo haki ya kupata elimu bora na hivyo kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi. Kufuatia tukio hili, Umoja wa Nchi Huru za Afrika iliazimia kuwa tarehe 16 Juni ya kila mwaka iwe Siku ya Mtoto wa Afrika.
Dkt. Nchimbiakizungumza kwenye maadhimisho hayo amesema maadhimisho ya mtoto afrika ni fursa ya kutathimini utekelezaji wa Sera za Taifa zinazohusu maendeleo ya mtoto kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwa ni pamoja na afya, elimu, ulinzi na malezi bora ili wawe tunu ya taifa na familia kwa ujumla, Kauli mbiu ikiwa UCHUMI WA VIWANDA TUSIMUACHE MTOTO NYUMA. Elimu bora utegemea afya bora yake (Miwani ni Tiba).
Aidha Dkt. Nchimbi amewataka wazazi kuwajali na kuwapenda watoto wao kwani waliwaleta duniani kwa mapenzi yao wenyewe yawapasa kuwalea na kuwakinga na ukatili wa kijinsia. Ameongeza kwa kusema wazazi wanawajibika kikamilifu katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu, kuwalinda na ukatili wa kijinsia pamoja na kupinga ndoa za utotoni ambazo zinawakatisha watoto masomo.
Katika sherehe yamaadhimisho ya mtoto Afrika, pia Dkt Nchimbi amezindua upimaji wa macho na chanjo ya mtoto pamoja na kuchangia Shilingi laki moja (100,000) ili watoto wapimwe macho na miwani
Vile vile Dkt Nchimbi amegiza shule zote za sekondari mkoani Singida kulima heka moja ya alizeti, kuandaa bwawa la samaki, kujenga na kukarabati chumba kimoja cha maabara na ameahidi kutoa zawadi ya pikipiki kwa shule nne zitakazo ongeza ufaulu mkoani singida.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.