Msaada wa Matandiko ambayo yamekabidhiwa kwa Mkuu wa mkoa wa singida Mhe: Dkt Rehema Nchimbi kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi kizega, Wilayani Iramba mkoani Singida.
matukio mbalimbali kwenye ziara ya Mkuu wa mkoa wa singida Mhe: Dkt Rehema Nchimbi kutembelea wanafunzi wenye mahitaji maalum na kukabidhi matandiko kwa ajili ya mabweni shule ya msingi kizega, Wilayani Iramba mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa singida Mhe: Dkt Rehema Nchimbi amefanya ziara ya kutembelea wanafunzi wenye mahitaji maalum na kukabidhi matandiko kwa ajili ya mabweni shule ya msingi kizega, Wilayani Iramba mkoani Singida.
Mhe: Dkt. Nchimbi ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Iramba Mhe: Emmanuel Luhahula, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Mwl. Godfrey Mwanjala na Viongozi mbali mbali wa wilaya ya Iramba.
Akizungumza na wananchi na wanafunzi hao Mhe: Dkt. Rehema Nchimbi amewashukuru sana shirika la World Vision msaada wa Magodoro 96, Mashuka na foronya zake 192 Mito 96 pamoja na Neti za kujikinga na mbu 96 vyenye thamani ya Tsh. 11,472,000/= pamoja na kushirikiana na jamii kwa kujenga vyumba 2 vya madarasa, ukumbi mmoja na tanki la kuvunia maji ya mvua. “Tumaini kwa msaada huu, utasaidia kuendelea kuboresha miundombinu ya shule ikiwemo elimu bora na ufaulu kwa wanafunzi kwa ujumla. Tunaweza kuona ni world vision wanameleta lakini kwa namna imeletwa kwa vijana hawa wenye mahitaji maalum, watoto wa mungu hawa ambaye mungu wametaka waishi na kufurahia maisha kwa makusudi yake mungu mwenye. Hivi vilivyoletwa kupitia na world vision vimeletwa na mungu
Nawashukuru sana shirika la World Vision, mumekuwa waaminifu kwa miaka mingi. Na mungu amewatumia kwa namna ya kipekee kwa namna mbalimbali kwa muda mrefu. Pongezi kubwa sana shirika la World Vision, tunawafadhili wengi, tuna Wadau wengi wa maendeleo, katika orodha hiyo shirika la World Vision mpo tena kwenye nafasi ya juu”. Alisema Dkt Nchimbi
Aliongeza kusema “nakusifu na kusema ukweli huu ili ujitambue ujue wewe nafasi yako ipi na umuhimu wako ni upi, sio kwamba mnacho au shirika la World Vision mnavyo, hapana nyinyi ni mkono wa mungu ambao unatumika kutufikia watu wenye mahitaji mbalimbali, kwahiyo mnaporatibu Mipango yenu, na kuweka na kalenda zenu wakati wote mjue kwamba, msifanye yote hayo maamuzi kama binadamu, mtangulizeni mungu katika ratiba na Mipango yote mtakayoifanya.
Dkt. Nchimbi ameomba shirika la World Vision kujenga Hosteli katika shule ya msingi kizenga kwa ajili ya wanafunzi hao “ninatamani maana wanaoishi hostel ni wanafunzi hawa wenye mahitaji maalumu, natamani tungekuwa na hostel kwa wanafunzi wote wa shule ya kizega, tunaweza pia turatibu kujua idadi ya wanafunzi ambao wanaweza kuingia kwenye shule hii, ili liwezekana, itasaidia kutengeneza utamanduni na tafsiri za maisha ya umoja na upamoja wa wanafunzi na watoto wote, maana watakapo kuwa hostel, na hawa wengine ambao hawana mahitaji maalum, kuna namna wataishi na kuweza kusaidiana vitu mbalimbali na hatimaye kupunguza makari ya ulemavu, maana hawa wakiwa pamoja, ni raisi kuonesha kwamba iki kinawezekana, hata kama kuna mlemavu ambaye anaona hawezi, na kukata tamaa. Alisema Dkt Nchimbi
Nyinyi shirika la World Vision kilichowasukuma na wakati wote mumeishi kwa kuonyesha upendo mkubwa, Thamani ya utu na asa kwa watu wenye huitaji maalum, hicho ndicho ambacho tunahitaji kipandwe na kipandikizwe na kilelewe kwa watanzania wote na ndani ya wanafunzi hawa na wakiwa wadogo kwani wananfunzi hawa ndo watakuwa Viongozi na watumishi wa mungu, tukiwaweka hawa pamoja tutapanda mbegu ya uhakika miongoni mwao.
Dkt Nchimbi ameagiza shirika la Tanesco na REA kuhakikisha wanafunga na kuwasha umeme katika shule ya msingi kizega. “Naagiza Tanesco na REA leteni umeme hapa, hakuna maelekezo mengine, leteni umeme hapa kwenye shule yenye uhitaji maalum, uwezi kupeleka sehemu nyingine ukakataa kuleta umeme kwenye watu hawa wenye mahitaji maalum. Pakiwa na umeme ni rahisi kuona na kuonana hata kama tumeweka ulinzi wa kuwalinda na kuweka uzio lazima hii shule ifungiwe umeme, alisisitiza Dkt Nchimbi
Aliongeza kusema "Rea mumwekwa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa kuwafungia nishati ya umeme, lazima wafunge umeme katika shule hii na watakuwa na furaha kubwa sana. huduma nyingi hazipatikani hapa shuleni kwa sababu hakuna umeme Kuna machine mpya za watoto hawa amabao wanamatatizo ya kuona ambazo zinatumia umeme, lakini kwa kuwa hawana umeme hawawezi kutumia hizo machine.
Mhe; Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli anafanya mambo mengi sana na anaupendo mkubwa kwa watoto wenye mahitaji maalum, leteni umeme ili watazame taarifa za habari ili waeze kuona Rais wetu. Tunawanyima haki ya kuangalia taarifa za habari na mambo makubwa anayofanya Rais wetu kwa watoto na watanzania kwa ujumla. Tumechimba kisima ambacho kina maji ya kutosha kwa ajili ya shule hii lakini hayawezi kufika kwa sababu hakuna umeme wa kuyavuta mpaka hapa shuleni. Alisema Dkt Nchimbi
Serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe: Rais Dkt. John Pombe Magufuli inawapenda sana na ndo maana kabla kujenga uzio, tuliweka ulinzi mkubwa na tulijenga uzio ili muwe na maisha yenye furaha na yenye tija asa kwenye mafanikio yenu. Misaafu inasema binadamu tumeubwa kwa sura na mfano wa mungu, nyinyi ni watoto wa mungu, nyingi ni marafiki wa mwenyezi mungu, nyinyi ni wathamani sana na niwambie tu kama misaafu invyosema, anayekubariki naye atabarikiwa na anayekudharau naye atadharauliwa.
Akisoma taarifa fupi ya kukabidhi matandiko kwa ajili ya mabweni shule ya msingi kizega, mratibu wa mradi kisiriri adp ndg. Modest Kessy alisema Shirika la Maendeleo la World Vision, kupitia mradi wa maendeleo wa World Vision Tarafa ya Kisiriri lilianza rasmi mnamo mwaka 2003. Mradi huu unafanya kazi katika eneo la Tarafa ya Kisiriri lenye kata 5 na vijiji 19. Shirika la World Vision ni shirika la Kikristo lisilo la kiserikali na linajikita katika maeneo makuu matatu:
Mh mgeni rasmi, katika utekelizaji huo tunaongozwa katika maeneo yafuatayo
Mradi umekuwa ukishirikiana na jamii pamoja na wadau mbalimbali katika kuboresha maendeleo ya mtoto katika maeneo makuu 4 ya afya, elimu,utetezi pamoja na kuhimiza upendo na amani kwa jamii. Shughuli za maendeleo zinafanyika panapokuwa na utulivu wa maisha na usalama.
Katika kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu, shirika limekuwa likishirikiana na wadau mbalimbali na jamii katika ujenzi na uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu ili iweze kuwa chachu ya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Miundombinu hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule/vyumba vya madarasa, matanki ya kuvunia maji ya mvua,ofisi za walimu,vifaa vyaa kufundishia na mafunzo mbalimbali kwa walimu,kamati za shule na wanafunzi kupitia vilabu vyao mashuleni.
Shule hii ya msingi Kizega ni moja wapo ya shule ambazo shirika la World Vision limeshirikiana na jamii kwa kujenga vyumba 2 vya madarasa,ukumbi mmoja na tanki la kuvunia maji ya mvua. Shule hii ina jumla ya wanafunzi wanaoishi na ulemavu 48 na wanafunzi wasio na ulemavu 432 na kufanya jumla ya wanafunzi wote kuwa 480.
Aidha kwa kutambua umuhimu wa shule hii kuwa na wanafunzi waishio na ulemavu, World Vision kupitia maradi wa maendeleo wa Tarafa ya Kisiriri, ulipata ufadhili wa kugharamia upatikanaji wa magodoro,mito, neti na mashuka kwa ajili ya hosteli/mabweni yote ya shule ya Msingi Kizega. Msaada huo ulitokana wafadhili kutoka Uingereza mwezi January 2019, ambapo pamoja na mafanikio na changamoto nyingine, wafadhili walipata fursa ya kutembelea mabweni wanayolala wanafunzi pamoja na mabweni mapya ambayo bado yalikuwa hayajakamilika.
Kulikuwa na changamoto mbalimbali kwa mabweni ya zamani yaliyokuwa yanayotumika na hivyo serikali ilijenga mabweni mengine 2 ya wanafunzi 48 kila moja ili kukabiliana na changamoto za mabweni ya zamani ambapo hata hivyo mabweni hayo mapya yalishindwa kutumika kwa kukosa baadhi ya miundombinu muhimu kama matandiko, maji/mfumo wa maji na umeme katika majengo yote kwa ujumla.
Msaada huu tunaoutoa leo unagharimu julma ya Tsh. 11.472,000/= (Milioni kumi na moja laki nne na elfu sabini na mbili) kwa idadi/mchanganuo ufuato;
Magodoro 96
Mashuka na foronya zake 192
Mito 96 pamoja na
Neti za kujikinga na mbu 96
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.