Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Peter Joseph Serukamba amehamasisha na kuelimisha wananchi umuhimu wa kuendelea kupanda na kutunza miti katika shule ya sekondari Maluga Wilaya ya Iramba leo tarehe 14 Januari 2023.
Upandaji miti una mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira. Miti hulinda vyanzo vya maji na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Vile vile husaidia kunyonya hewa ukaa na hivyo kuchangia katika juhudi za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Akiongea na wananchi amesema, “Kwanza nichukue nafasi hii kuwashukuru mmejitokeza kupanda miti,nia yetu kila nyumba ipande miti minne na lazima tupande maeneo yote ya zahanati , vituo vya afya, shule zote za misingi na sekondari na kwenye barabara zote tupande miti
Ndugu zangu ninawahamasisha wananchi wote kuendelea kupanda miti hasa katika kipindi hiki cha mvua, kuitunza, na kuihifadhi, jambo hili ni la msingi sana, tunapanda miti kwa sababu tunataka kulinda mazingira yetu,tunapanda miti katika maeneo yetu kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo, tunapanda miti kwasababu ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, mabadiliko ya tabia nchi yameletwa na kazi zetu sisi wanadamu za ukataji wa miti usio endelevu, mioto kichaa, na upanuzi wa mashamba. Hivyo, ili kuziba pengo la miti inayopotea tunatakiwa tupande miti ya kutosha, tumesababisha kuwepo kwa joto kubwa duniani, kwa sasa hatupati mvua kama tulivyokuwa tunapokea, sasa tunalojukumu kurudisha tulichokifanya.Amesisitiza Mhe:Serukamba
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe: Suleiman Mwenda akipada miti katika shule ya sekondari Maluga
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Iramba Mhe: Samwel Shilla akipada miti katika shule ya sekondari Maluga.
Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Iramba Mhe: Innoent Msengi akipada miti katika shule ya sekondari Maluga.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Marietha Kasongo akipanda miti katika Shule ya Sekondari Maluga
Wananchi wakishiriki kupanda miti katika shule ya sekondari Maluga Wilayani Iramba.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.