MKUU WA MKOA WA SINGIDA PETER JOSEPH SERUKAMBA,AMEWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI WILAYANI IRAMBA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KIKAMILIFU.
Viongozi wa serikali katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida, wametakiwa kusimamia miradi ya Maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo,inamalizika kwa wakati.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Joseph Serukamba wakati wa ziara yake ya Siku mbili ya Kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo ya Iramba.
Katika ziara hiyo Mei 16,RC Serukamba amekagua miradi 16 ya Maendeleo inayotekelezwa katika Tarafa ya Ndago na Kinampanda ambapo miradi mingi imetekeleza na ipo katika hatua za mwisho huku miradi mingine ikiwa katika hatua za kati na RC Serukamba kuagiza viongozi wa Wilaya kuelekeza nguvu zao Ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Serukamba amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Gunnah Maziku kuelekeza macho yake,kwenye ujenzi wa Shule Mpya ya Ng'anguli itayogharimu jumla ya Tsh. Mil. 493.4 ambao mpaka sasa unasuasua,Huku Matundu ya Vyoo 24 hayajaanza kuchimbwa.
Pamoja na Serukamba kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji kuelekeza macho yake hapo lakini Bado Serukamba amemtaka Diwani wa kata hiyo ya Maluga Ramadhani Mbutu kuhakikisha Shule hiyo inakamilika kwa wakati uliopangwa na kumtaka Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Juveranice Sebastian kuachia Ngazi kama hawezi kusimamia kazi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.