Mkuu wa Wilaya Emmanuel J. Luhahula amefanya ziara katika shule ya Sekondari Mtoa iliyopo kata ya Mtoa, Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba na kuwakumbusha wanafunzi jukumu lao la msingi kuwa “Wazazi wanapokununulia sare, kalamu na madaftari wanahitaji matokeo mazuri, kila mmoja anamatajirio ya mbele na mungu awatangulie sana”
Aidha katika ziara hiyo Mhe, Mkuu wa Wilaya amepokea madawati sitini(60) yaliotengenezwa na serikali ya vijiji vinavyoizunguka shule na kuyakabidhi kwa kaimu mkurugenzi.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba akiwa katika Kijiji cha Masagi kata ya Mtoa, Tarafa ya Shelui amewataka wananchi kulinda amani ambayo ni tunu ya Taifa letu, tuache chokochoko za kugombea madaraka, tuhakikishe zahanati yetu tumeipaua kwa kuahidi kuchangia kiasi cha shilingi laki tano (500,000/=),amewaomba wazazi kuwapeleka watoto wote watakaofaulu shule, amewataka viongozi kuwakamata wote ambao hawajajenga vyoo na kuwapiga faini ya shilingi elfu hamsini (50,000/=) na kujenga choo, amewaomba wananchi waache kuwatunza wahamiaji haramu na kama wapo watoe taarifa mapema kwa Mkuu wa Wilaya, tuhakikishe tunapambana na rushwa kwa kutoa taarifa.
Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emanuel J. Luhahula akiwa katia ziara katika Kijiji cha Kinkunku kata ya Mtoa, Tarafa ya Shelui ameawaambia wananchi kuwa anakerwa na mauwaji yanayofanyika hapo, amewaomba wamuhakikishie kumpa taarifa ya wale wanaofanya mauwaji ili yeye atume askari na kuwakamata wauwaji hao, amewataka wanachi hao waache kutunza siri za kijinga,
Aidha amewaambia wananchi hao afurahishwi na kuwaozesha watoto “ ameagiza Maganga Mayala mzazi wa mtoto huyo,Juma Pili Njile muoaji na mlezi Juma Pili Kibanda wakamatwe wote wapelekwe mahakamani”Amewataka wananchi waimarishe amani “ Amani yetu ipo mikononi mwetu na kamwe watu wasijibanze katika mwamvuli wa dini kufanya ya hovyo, tuache kuanzisha chokochoko za kiimani”
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.