Profesa Idrisa Kikula Mwenyekiti wa Tume ya Madini Tanzania amefanya kikao katika Kijiji cha Nkonkilangi kata ya Ntwike Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba cha kuwaelimisha viongozi ngazi ya Wilaya hadi Kijiji na wachimbaji wadogo wadogo muundo wa Tume ya Madini, Majukumu yake na vitendea kazi vyake ambavyo ni :
1. Kuwataka wachimbaji wakati na wakubwa kuapa kufuata maadili ya kitanzania na kamwe hawataidanganya serikali ya Jamuhuri ya Tanzania na watafuata kadri sheria zanchi zinavotaka.
2. Serikali inawataka wachimbaji wakati na wakubwa kutumia watu na vituvinavyopatikana nchini kwetu.
3. Muungozo wa jinsi ya kuyalipia madini na namna ya kuyasafirisha
Aidha ametaja baadhi ya majukumu ya Tume ya Madini ambayo ni kusimamia sekta ya madini na kuahakikisha kwamba uchimbaji unafuata taratibu zake, kusimamia mapema utatuzi wa migogoro, kusimamia upatikanaji wa maduhuli ya serikali, kuishirikisha serikali kuanzia ngazi ya wilaya hadi Kijiji katika kuyatekeleza majukumu hayo, kusimamia unufaikaji wa jamii inayozunguka eneo la uchimbaji na ukusanyaji wa stahiki za serikali kwa kuweka takwimu sahihi.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emanuel J. Luhahula amewaeleza viongozi wa wachimbaji wadogo wadogo wa Nkonkilangi kata ya Mtwike Tarafa ya Shelui wilayani Iramba, ambao hawajapata leseni wafuate utaratibu wa kupata leseni hizo, amewataka waunde vikundi vyao ili ushirika wao ukae vizuri, walipe mapato yao serikalini, pia amewaomba wadumishe amani, amani ibaki na iweze kupatikana maeneo hayo ya machimbo.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.