Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewaagiza Maafisa Elimu Kata kuendelea kusimamia kwa ukaribu shule zilizopo katika kata zao ili kuinua ufaulu wa Wanafunzi katika shule zilipo Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.
Luhahula ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 8, 2021 katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo wakati akigawa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu vizuri mtihani wa darasa la saba na kupangiwa shule mbalimbali Nchini.
“Tunataka hamasa hii ya ugawaji wa zawadi iwainue wanafunizi wote kitaaluma na kufaulu mitihani yao hatimae kuinua Iramba yetu” amesisitiza Mkuu wa Wilaya
Kufuatia Maafisa Elimu Kata kupata posho ya Madaraka na kugawiwa pikipiki kwa lengo la kufanikisha usimamizi wa shule zilizopo katika kata zao, amewagawia mataili ya pikipiki hizo na kuwaasa kuzitumia pikipiki hizo kuzunguka katika maeneo yao kusimamia taaluma.
“Hakikisheni mnazunguka katika kata zenu na kusimamia yale yote tuliyokubaliana katika kikao cha Wadau wa Elimu Wilayani Iramba.”
Pia amewataka Maafisa Elimu Kata hao kuhakikisha wanakua na utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi wanaowazunguka katika kata zao.
Awali akiwasilisha taarifa fupi ya wanafunzi waliofaulu vizuri na kuzawadiwa zawadi zilizoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri, Chacha Kehogo amesema kuwa wanatoa zawadi kwa wanafunzi waliofaulu vizuri na kuwapatia Maafisa Elimu Kata vitendea kazi kwa lengo la kuhakikisha wanasimamia taaluma kwa ukaribu katika kata zao.
“Tumetoa mataili 40 kwa Maafisa Elimu Kata ili kuwawezesha kuzunguka na kufuatilia taaluma katika shule zao,” amesema Kehogo na kuongeza kuwa
“Ufaulu mzuri walioupata wanafunzi 10 katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2020 umewawezeshesha wanafunzi hao kupangiwa shule nzuri Nchini.”
Kehogo amebainisha kuwa mwanafunzi Raphael Maganza amepangiwa Tabora Boys, Benedict Isaya amepangiwa Kibaha, Vailet Jackosn amepangiwa Tabora Girls, Gwakisa Mwakijungu amepangiwa Mzumbe na Sixbert Sabigoro amepangiwa Ilboru.
Wakati Yunusu Swalehe amepangiwa Iyunga Technical, Mary Mkumbo amepangiwa Msalato, Benson Makule amepangiwa Ifunda Technical, Gift Kileo amepangiwa Mtwara Technical na Saada Mnyinga amepangiwa Balangdalalu.
Akiongea na Mwandishi wetu mmoja wa wanafunzi waliopewa zawadi kwa niaba ya wenzake Gift Kileo amewashukuru viongozi wa Wilaya ya Iramba kwa kufanikisha zoezi la utoaji wa zawadi ambazo zitasabisha Wanafunzi hao wafikie ndoto zao.
“Kwa kweli tunashukuru kupata zawadi hizi na kwa shule tulizopangiwa tunamatumani makubwa ndoto zetu zitatimia” amesema Kileo na kuongeza kuwa
“Ninaamini zawadi hizi tulizopewa zitatusaidia katika masomo yetu huko tuendako.”
Kwa upande wake mmoja wa wazazi waliohudhuria hafla hiyo fupi, Vaileti Mbigu amewaasa wazazi wenzake kuwalea na kuwatunza wanafunzi waliopo katika shule mbalimbali ili waweze kutimiza ndoto zao.
“Niwaombe wazazi wenzangu tuwatunze na kuwaelekeza watoto wetu vizuri wanapokua katika hatua mbalimbali za masomo na katu tusiwakatize ndoto zao,” ameomba Mbigu na kuongeza kuwa
“Niwaombe mfahamu kuwa watoto hawa ni mali ya Taifa na watakuwa na uwezo wa kulinda Taifa letu kwa kutumia maarifa wanayoyapata na watakayo yapata katika elimu ya juu.”
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula agawa mataili ya pikipiki 40 kwa Maafisa Elimu Kata na kuwataka kwenda kusimamia taaluma kwa ukaribu ili kuinua taaluma na ufaulu Wilayani Iramba Mkoa wa Singida. Wakwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula, wakatikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni na wamwisho kushoto ni Afisa Elimu Msingi wa Halmashuri hiyo, Chacha Kehogo.Picha na Hemedi Munga
Afisa Elimu Msingi, Chacha Kehogo akifafanua wanafunzi waliopangiwa shule mbalimbali Nchini, ambapo mwanafunzi Raphael Maganza amepangiwa Tabora Boys, Benedict Isaya amepangiwa Kibaha, Vailet Jackosn amepangiwa Tabora Girls, Gwakisa Mwakijungu amepangiwa Mzumbe na Sixbert Sabigoro amepangiwa Ilboru. Wakati Yunusu Swalehe amepangiwa Iyunga Technical, Mary Mkumbo amepangiwa Msalato, Benson Makule amepangiwa Ifunda Technical, Gift Kileo amepangiwa Mtwara Technical na Saada Mnyinga amepangiwa Balangdalalu. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akiwaasa wanafunzi waliochaguliwa kwenda shule mbalimbali Nchini kuto iga tabia za wale watakaokutana nao, vitu vyao na kuridhika na kile watakachokuwa wanapewa na wazazi wao. Alio kaa ni Afisa Elimu Msingi Chacha Kehogo. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mbalimbali waliochaguliwa katika shule mbalmbali Nchini. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Elimu Kata. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.