Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula ameihakikishia timu ya Karantini, Wataalam na Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Iramba kuwa vifaa vyote vinavyohitajika katika kupambana na kuchukua tahadhari ya maambukizi ya ugonjwa wa corona havitapungua.
Luhahula ameyasema hayo leo Jumaa tano Aprili 22, 2020 wakati akiongea na timu ya karantini kuwatia moyo katika Ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
Mkuu wa Wilaya hiyo amewaagiza wataalam kuainisha vifaa vyote vinavyohitajika.
“ Tutafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kuwa vifaa ambavyo ni vya timu yetu iliyo mstari wa mbele havitapungua” amesisitiza Luhahula
Katika hatua nyingine, Luhahula amewashukuru watu wa Afya kwa ubunifu wa kutengeneza barakola kwa ajili ya jamii.
Pia amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo kutoa maelekezo kwa taasisi zilizo chini yao kutengeneza vitu vya kunawia ambavyo havishikiwi na mkono.
“Ninaiomba timu ya karantini kuwekeza zaidi kwenye kinga kwa kuwa ndio usalama wetu ulipo, hivyo ninawatia moyo na tuendelee kumtegemea mungu,” amesema Luhahula na kuongeza
“ Ninaamini kuwa tukishikamana katika haya mapambano Mungu wetu atatusimamia.”
Halikadhalika amewataka viongozi wa timu hiyo kuratibu mambo yote mapema huku akiwatahadharisha wale wote watakao kua kikwazo au kuzembea kwa ajili ya wapiganaji hao kumchukulia hatua za kinidhamu mara moja.
“ Ndugu zangu nawatia moyo twendeni tukafanye kazi na tuwe na moyo mkuu,” amesisitiza Luhahula
Akiongea katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni amewasisitiza Watendaji wa Kata na Vijiji kuendelea kuzibaini familia ambazo zinaingia katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu kutoka mikoa mbalimbali.
“ Ninawakumbusha Watendaji wa Kata na Vijiji kuwa na takwimu za watu wanaokuja ili likitokea jambo iwe rahisi kufuatilia,” amesema Mwageni
Mapema akiwasilisha taarifa fupi mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Daktari Hussein Sepoko amemuhakikishia Mkuu huyo kuwa mpaka leo hii Wilaya ya Iramba haijapata muhisiwa wa ugonjwa wa corona ambaye amechukuliwa sampuli.
Sepoko amesema kupitia mikakati walioiweka katika timu ya karantini wameweza kupata Themo scana 5 ambazo zinatumika huku Idara ya Afya ikinunua spriers 8 kwa ajili ya upuliziaji.
Kuendelea kufikisha elimu ya ugonjwa wa corona katika maeneo hatarishi kama vile sehemu za bodaboda, minadani, machimboni, Doromoni kwenye uvuvi wa samaki, nyumba za ibada na kwenye Misiba.
“ Pia, tumefanya oparesheni katika stendi zetu za mabasi na kukuta wameweka sanitaiza na kufanya uchunguzi (screening) pindi mabasi yanapoingia toka mikoani,” amesema Sepoko
Naye Mjumbe wa Timu ya Karantini ya Wilaya hiyo, Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Kiomboi, Noela Vicent ameshauri kuwa watu wote wanaokuja kuona wagonjwa wawe wamevaa barakola.
Kwa upande wake Mratibu wa uimarishaji ubora wa huduma za Afya wa Wilaya hiyo, Daniel Paulo ameishauri kamati hiyo kuwafanyia uchunguzi wageni wote watokao mikoa yenye maambukizo.
Pia ameitaka jamii kuendelea kunawa kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni sahihi.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akifafanua jambo wakati akiongea na timu ya karantini ya Wilaya hiyo. Picha na Hemedi Munga
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Daktari Hussein Sepoko akitoa taarifa ya utekelezaji wa timu ya karantini ya Wilaya hiyo Mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo. Picha na Hemedi Munga
Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Kiomboi, Noel Vicent, akichangia mada katika kikao cha timu ya karantini kilichofanyika ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
Mratibu wa Uimarishaji Ubora wa Huduma za Afya wa Wilaya ya Iramba akichangia mada katika kikao cha timu ya karantini kilichofanyika ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
Wajumbe mbalimbali wa timu ya karantini wakifuatilia uchangiaji taarifa ya timu hiyo ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
Mfano mzuri wa chombo cha kanawia bila ya kushika kwa mikono. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akinawa maji yanayotiririka toka katika chombo kinachobonyezwa kwa mguu kutoa maji na upande mwingine kutoa sabuni. Picha na Hemedi Munga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Songoma akinawa maji yanayotiririka toka katika chombo kinachobonyezwa kwa mguu kutoa maji na upande mwingine kutoa sabuni. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akinawa maji yanayotiririka toka katika chombo kinachobonyezwa kwa mguu kutoa maji na upande mwingine kutoa sabuni. Picha na Hemedi Munga
Mganga Mkuu wa Halamashauri ya Wilaya ya Iramba, Daktari Hussein Sepoko akinawa maji yanayotiririka toka katika chombo kinachotumiwa kwa mguu kutoa maji na upande mwingine kutoa sabuni. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.