Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amefanya ziara ya kushitukiza kukagua utekelezaji wa Mpango wa kuhamasisha Walengwa wa kuweka akiba na kuwekeza unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kijiji cha Zinziligi Tarafa ya Ndago Wilayani Iramba.
Mkuu wa Wilaya amefanya ziara hiyo leo Jumatatu Machi 2, 2020 kijiji cha Zinziligi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.
Akiwa katika kijiji hicho, Luhahula amewaambia walengwa wanaonufaika na MfuKo wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuwa kiasi ambacho watapewa baada ya kuunda vikundi vya ujasiriamali kuhakikisha wanakitumia vizuri kiasi hicho.
Halikadhalika amewahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa suala la maji litapata ufumbuzi muda mfupi ujao.
“Ndugu zangu ninapenda kuwahakikishia kuwa mwezi wa tatu mwaka huu gari litakuja kuanza kuchimba visima kwa ajili yakupata maji,” amesema Luhahula
Naye Mkuu wa Kupambana na kuziwia rushwa (TAKUKURU) Wilayani Iramba, Ahmed Sungura amewaeleza wanufaika hao kuwa wanao wajibu mkubwa kuendeleza mapambano zidi ya rushwa.
“Ninaomba mtambue kuwa mapambano zidi ya rushwa sio ya TAKUKURU peke yake ni ya jamii nzimani kwani rushwa inatugusa sote kama jamii,” amesema Sungura na kuongeza
“ Tuhakikishe jamii inasimamia vizuri miradi inayotolewa na serikali pamoja na kuilinda na kuisimamia.”
Sungura ametumia ziara hiyo kutoa elimu ya rushwa na kuwataka wananchi hao kutoa taarifa TAKUKURU pindi wanapoona kuna miradi haiendi sawa na hakuna uwazi.
Amewataka wananchi hao kutofumbia macho rushwa kubwa zinazohusu viongozi wakubwa wenye mamlaka makubwa, rushwa ndogo zinazohusu viongozi wa chini na rushwa ya ngono.
“Mapambano zidi ya rushwa ni jukumu la kila mtu, tushirikiane kutokomeza rushwa,” amesisitiza Sungura
Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo, Anania Mbuta amesema mafunzo hayo yemelenga kuwawezesha wanufakia wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini(TASAF) kuweza kuunda vikundi vya ujasiriamali vitakvyo wawezesha kuweka akiba na kuwekeza.
Mafunzo ya awali kwa vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Iramba.
MWISHO
Mkuu wa Kupambana na kuziwia rushwa (TAKUKURU) wilayani Iramba, Ahmed Sungura akiwaeleza wanufaika wa Mpango wa kuhamasisha Walengwa wa kuweka akiba na kuwekeza unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kijiji cha Zinziligi Tarafa ya Ndago Wilayani Iramba kuwa wanao wajibu mkubwa kuendeleza mapambano zidi ya rushwa. Picha na Hemedi Munga
Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kuhamasisha Walengwa wa kuweka akiba na kuwekeza unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kijiji cha Zinziligi Tarafa ya Ndago Wilayani Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.