By Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni kwa kulipa deni la ujenzi wa Zahanati ya Ushora.
Luhahula ameyaongea hayo leo Ijumaa Novemba 29, 2019 katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri hiyo wakati wakiwa katika kikao cha tathimini ya mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo 2019.
Akiongea katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya hiyo, amewataka wanakamati wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 kuendelea kujifunza kwa kuwa wamefanya kazi kubwa mpaka Mwenge wa Uhuru ukapita salama bila ya kuacha majeraha kwa watumishi.
Huku akibainisha kuwa kufanya tathimini ni kutathimini majukumu ambayo tulipewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambapo balada yakuja yeye anatuma Mwenge wa Uhuru kupita katika kila Halmashauri kukaguwa kama wale waliopewa majukumu wanawajibika ipasavyo.
Mkuu wa Wilaya hiyo ametumia kikao hicho kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kupeleka 3.6 milioni kulipa deni la ujezi wa Zahanati ya Ushora.
Akitoa taarifa ya matokeo ya Mwenge wa Uhuru 2019, Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Wilayani Iramba, Romwald Mwendi amesema Iramba imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika uraghabishaji wa falsafa ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi.
Mwendi amesema matokeo ya jumla kimkoa, Iramba imeshika nafasi ya sita wakati Wilaya ya Mkalama ikishika nafasi ya mwisho huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Wilaya ya Itigi, nafasi ya pili Wilaya ya Manyoni, nafasi ya tatu Singida Vijijni , nafasi ya nne Wilaya ya Ikungi wakati nafasi ya tano ikishikwa na Singida Manispaa.
Hata hivyo amebainisha nafasi iliyoshika kitaifa ambapo Iramba imekuwa ya 174 wakati Wilaya ya Mkalama imekuwa ya 184 huku Wilaya ya Itigi ikishika nafasi 93.
Akichangia katika tathimini hiyo Afisa wa kuzuwia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Benjamini Masyaga amewakumbusha wanakamati wote wa Mwenge wa Uhuru 2019 kuwa wanapopewa majukumu wanapaswa kujiongeza na kuhakisha wanakuwa na mawasiliano yakutosha.
Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Wilayani humo, Mwakijungu ameshauri taarifa ya fedha kutaja malengo ya kila kijiji au kata yaliotakiwa kufikiwa huku akiwataka wenyeviti wakamati zote kuwepo kikao kijacho ili wajadili kwa pamoja.
Mwenge wa Uhuru 2019 Wilayani Iramba ulikimbizwa kilometa 142.5 hadi eneo la makabidhiano Wilayani Igunga , ulipitia katika Tarafa 3 , kata 7 na vijiji 14 huku ukipitia miradi 4 na shughuli sita ambapo miradi yote na shughulizi zote zilikuwa najumla ya garama ya 1.1 bilion.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zilifikia kilele Oktoba 14, 2019 siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana zilizofanyika uwanja wa Ilulu Mjini Lindi.
Baadhi ya wajumbe wa kamati za Mwenge wa Uhuru 2019 wakifuatilia tathimini ya Mwenge ukumbi mkubwa wa Halmashuri ya wilaya ya Iramba. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.