Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewaagiza Maafisa Tarafa na Maafisa Elimu Kata kuwakamata wazazi ambao hawajapeleka watoto shule.
Agizo hilo amelitoa leo Ijumaa Machi 13, 2020 wakati akiongea katika kikao cha Baraza la Madiwani Ukumbi Mdogo wa Halmashauri hiyo mjini hapa.
“ Kamata wazazi ambao hawataki kupeleka watoto wao shule, tunataka Iramba yetu isonge mbele na haiwezi kusonga mbele kama watoto wetu hawapati elimu,” amesisitiza Luhahula
Pia amewataka Madiwani hao kuendelea kuhamasisha wananchi kutoka maeneo ya mabonde huku akiwapongeza kwa namna ambavyo wanavyosimamia miradi ya maendeleo.
“ Niwaombe tuendelee kuonesha uadilifu katika kusimamia miradi ya maendeleo na kukifanya kituo cha Afya Shelui kuwa kituo bora,” amesisitiza Luhahula
Halikadhalika amewataka Madiwani hao kuhamasisha kulima mazao yanayokabiliana na hali ya mvua inayoendelea kunyesha.
Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Simion Tyosela amemuhakikishia Diwani wa Kata ya Shelui, Kinota Hamisi kuwa Halmashauri hiyo itakuwa pamoja katika ujenzi wa kituo cha Afya Shelui.
Tyosela amewataka Madiwani hao kuendesha kampeni ya kupinga mimba na utoro kwa wanafunzi waliopo katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni amewashukuru Madiwani hao kwa ushirikiano wao katika kujadili mambo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa mapato kwa mustakabali wa maendeleo ya Wilaya ya Iramba.
Naye kaimu Afisa Ardhi na Maliasili wa Halmashauri hiyo, Lugano Sanga amewaomba Madiwani wa Baraza hilo kufahamu kuwa wataalamu wanapokwenda kupima mipaka ya maeneo mbalimbali hawampendelei yoyote bali wanafuata ramani.
MWISHO
kaimu Afisa Ardhi na Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Lugano Sanga akifafanua mambo yanayohusu ardhi na mipaka yake wakati wa Baraza la Madiwani. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.