Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewaomba viongozi wa dini kuisaidia serikali kufikisha ujumbe wa chanjo ni kinga kwa pamoja tuwakinge.
Mkuu wa Wilaya, Luhahula ameyasema hayo katika kikao cha mafunzo ya kampeni ya chanjo ya surua, rubella na chanjo ya polio katika ukumbi wa Halmashauri leo septemba 26, 2019.
Akiongea na kamati ya kampeni, amewataka watendaji wote kwenda kuhamasisha na kuelimisha kampeni ya kuwakinga na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ya ugonjwa wa surua, rubella na polio.
“Kinga ni bora kuliko tiba, nibora tukinge maana tunapokinga tunaandaa Taifa zuri katika wilaya ya Iramba na kujenga Taifa zuri tunalolipeleka kwenye uchumi wa kati na uchumi wa viwanda” Alisema Luhahula
Akiongea katika mafuzo hayo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida Tanzania, Hussen Sepoko amesema kuwa lengo la kampeni ni kuwakinga na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ya ugonjwa wa surua, rubella na polio.
Mganga Mkuu, Sepoko amesema kuwa kampeni hii itafanyika nchi nzima katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya mama na mtoto na maeneo yote ya chanjo tembezi na chanjo mkoba.
Naye Mratibu wa Chanjo Wilaya ya Iramba, Jackson Shillah amesema kuwa wajibu wa viongozi katika ngazi zote ni kuhakikisha , wanaelimisha na wanahamasisha jamii ili kuwafikia watoto wote.
Akibainisha wakati wa mafunzo hayo kuwa wanatarajia kuchanja jumla ya watoto 37,261 kwa chanjo ya surua na rubella huku watoto 20, 534 wakichanjwa chanjo ya sindano ya polio katika wailaya ya Iramba.
Shillah alieleza kuwa chanjo ya surua na rubella ni kwa ajili ya watoto wote wenye umri kuanzia miezi 9 hadi chini ya umri wa miaka 5.
Wakati chanjo ya polio ni watoto wote wenyekuanzia umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na nusu.
Aidha amewataka viongozi kuelimisha jamii juu ya ubora na usalama wa chanjo kwa watoto na kuelimisha juu ya umri sahihi wa kupata chanjo ya surua, rubella na polio.
Huku akiwataka viongozi kukanusha upotoshaji na uvumi wa aina yeyote kuhusu chanjo hizi kwa kuwa chanjo hizi ni salama na hazina madhara yoyote.
Akichangia mada katika mafuzo hayo Makamu Askofu Jimbo la Singida Kaskazini, Robert Kijanga amewaomba wakuu wa idara wote wawe huru kufika katika maeneo ya ibada ili wawaelimishe hata kama itakua ni upande wa mipango na miradi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Simion Tyosela akichangia mada wakati wa majadiliano katika mafunzo ya kampeni ya chanjo ya surua, rubella na polio. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wakati kulia mwa Mwenyekiti ni Mganga Mkuu Hospitali ya Kiomboi Iramba, Hussen Sepoko. Picha na Hemedi Munga.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.