Hemedi Munga, Irambadc
Iramba. Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula amewashukuru Wadau wote kwa kuchangia takriban Tsh 14.6milioni kwa ajili ya kununua vifaa vya kuchukua tahadhari ya maambukizi ya homa kali inayosababishwa na virusi vya corona Wilayani Iramba.
Shukrani hizo amezitoa leo Juni 10, 2020 wakati alipokutana na baadhi ya Wadau katika viwanja vya Mkuu wa Wilaya hiyo mjini hapa.
“Niwashukuru Wadau wote kwa kuitikia wito, hivyo mmeonesha namna gani wananchi wa Iramba mnavyojali, ninawaomba wakazi na wasiowakazi wa Iramba kukumbuka kuwa Iramba ni yakwenu hivyo nilazima tuwekeze,” amesema Luhahula na kuongeza
“Ninawaomba wakazi wote wa Iramba na wale wasio wakazi wa Iramba ambao wako tayari kuwekeza wakaribie eneo la Salala kuna hekari 113 za kujenga matawi ya vyuo vikuu.”
Eneo la Salala lililopo njia kuu ya kuelekea Misigiri barabara kuu itokayo Singida mjini kuelekea jijini Mwanza lipo wazi kwa ajili ya mpango mahususi wa kuufanya mji wa Iramba kuwa Mji wa kisasa maana maeneo hayo tutaweka vituo vya Afya, Sheli na shule huku akiwataka wale wenye ndugu nje za nchi kuwaambia ndugu zao kuja kuwekeza Iramba.
Halikadhalika, amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni kuhakikisha kitanda cha kujifungulia kilichototewa na ndugu Amoni aliyewakilishwa na ndugu yake, Winjuka kinapelekwa Zahanati ya Misigiri ili kukidhi utashi wa mfadhili.
Akiongea baada ya kukabidhiwa vifaa vya kuchukua tahadhari ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Linno Mwageni amewashukuru Wananchi kwa kuwa na muamko wa kuchangia kuiunga mkono Serikali inayoongonzwa na Rais wetu, Dkt John Magufuli.
Aidha amempongeza sana ndugu Winjuka kwa kuwakumbuka wakinamama kutoa kitanda ambacho watatumia wakati wa kujifungua.
“Nikushukuru sana dada Winjuka kwa kuwakumbuka wakinamama wanavyopata tabu maana ukimlinda mama tayari unakua umeilinda jamii,” amesema Mwageni
Kwa upande wake mmoja wa Wadau hao, Ndugu Winjuka akitoa shukrani kwa niaba ya Wadau wote amesema wanaishukuru Serikali kwa kukubali wao kuwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Winjuka amesema kwa niaba ya ndugu yake aliyopo nje ya Tanzania wameweza kuchangia takriban Tsh 2.6milioni ambazo zimeweza kununua kitanda cha kujifungulia (delivery bed), PPE na vitakasa mikono (sanitizer).
MWISHO
Ndugu Winjuka akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula baadhi ya vifaa alivyochangia kuunga mkono juhudi za Mhe, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli dhidi ya mapambano ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. Picha na Hemedi Munga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Linno Mwageni akishika kitanda cha kujifungulia kilichotolewa na ndugu Winjuka kwa ajili ya Zahanati ya Misigiri ili kuwawezesha akina mama kujifungua kwa usalama. Picha na Hemedi Munga
Afisa Elimu kata ya Ulemo na Mratibu wa andiko lililosababisha kupatikana kwa vifaa hivi wakwanza kushoto, Nickson Mmanyi akishirikiana na Ndugu Winjuka kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Emmanuel Luhahula kitanda na kipima joto (thermo scanner) kwa ajili yakusaidia huduma za afya na mapambano ya kuchukua tahadhari ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. Picha na Hemedi Munga
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba, Pius Songoma akikagua vifaa vilivyotolewa na Mdau Winjuka. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.