Hemedi Munga, Irambadc
Iramba.Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula amezindua mradi wa maji Gereza la Ushora.
Luhahula amezindua mradi huo leo Ijumaa Januari 03, 2020 katika Gereza la Ushora lililopo Tarafa ya Ndago Wilayani Iramba.
Akiongea katika hafla hiyo, luhahula amempogeza Rais wa wa Tanzania , Dtk. John Magufuli kwa kutoa Bilioni 1 na milioni mia tano kumi na nne kwa wilaya ya Iramba pekee kwa kipindi cha miaka mine kutekeleza miradi ya maji.
Huku akieleza mafanikio ya upatikanaji wa maji kufikia 53.6% ukilinganisha na wakati anaignia madarakani upatikanaji wa maji ulikuwa asilimia 43%.
Akibainisha malengo ya serikali katika kutimiza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kumtua mama ndoo kichwani kwa kuweka vituo vya kutolea maji (DP) kila umbali wa mita 400.
Aidha amemuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singda, Msekwa Omari kuhakikisha wanapanda miti kulinda uwoto wa asili wa vyanzo vya maji ushora.
Akimkaribisha mwekezaji Profesa Giuseppe kutoka Italia, mwakilishi wa wizara ya maji, Lidya Joseph amemshukuru mwekezaji huyo kwa kutatuwa tatizo la maji katika jamii ya watu wa Ushora.
Akiongea katika hafla hiyo profesa Giuseppe amesema kusherehekea kukamilika mradi huo ni kusherehekea maisha huku akiwataka kufahamu kuwa 90% ya mwili wa mwadamu umeumbwa na maji.
“ Tunatokea kwenye maji, kiumbe cha kwaza kugundulika ilikuwa ni bakteria kutoka kwenye maji na tunapojifunza sayari zilizoko karibu nasisi tunaangalia uwepo wa maji kuona uwezekano wa maisha” Alisisitiza Giuseppe
Mapema akisoma taarifa ya mradi wa maji Gereza la Ushora meneja wa maji RUWASA wilayani humo, Ezra Mwacha amesema mradi umegharimu 89.1 milioni, huku akifafanuwa kuwa 78.2 milioni zinatoka kwa wadau wa maendeleo “Rotary Club Rho” wa Italia na 10.8 milioni kutoka Magereza, Ofisi ya katibu Tawala Mkoa wa Singida na Halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Fedha hizo ziliwezesha kufanya utafiti wa maji ardhini na uchimbaji wa kisima kirefu cha mita 115 chenye uwezo wa kuzalisha wingi wa maji wa lita 5,600 kwa saa.
Mwacha ameeleza miundombinu iliyojengwa kuwa ni ujenzi wa vituo 8 vya kuchotea maji (DP), ujenzi wa mnara wa mita sita, kununua na kuweka tanki la plastiki lenye ujazo wa lita 10,000, ujenzi wa fensi na jengo moja la mitambo ya kuendeshea pampu, kulaza, kuunganisha na kufikia mtandao wa mabomba wenye urefu wa mita 2,575.
Kufanikiwa kwa mradi huo kumefunguwa nafasi ya ketekeleza maagizo ya Rais wa Tanzania, Dtk. John Magufuli ya kuwataka magereza kuzalisha chakula kwa wingi.
Naye Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida, Msekwa Omari ameeleza kuwa Gereza la Ushora ndio gereza linalotegemewa kwa chakula na magereza yote Mkoa wa Singida.
“ Baada ya maji kupatikana nguvu kazi ya wafungwa itatumika katika shughuli za uzajishaji,” alisibitisha Omari
Huku akiahidi kuulinda mradi huo ili udumu kwa muda mrefu kuendelea kupata matunda yake.
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iramba, Ibrahimu Mjanaheri amempogeza Profesa Giuseppe kwa kusogeza huduma ya maji ambayo ndio chanzo cha kuondoa magonjwa yanayoweza kusababishwa na ukosefu wa maji safi na salama.
“ Unapoleta maji mahala unaondoa magonjwa ambayo yanaonyemelewa na ukosefu wa maji,” alisema Mjanaheri
Kwa upande wake mnufaika wa maji yatokanayo na mradi huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Utemini, Mwanaisha Mfaume amesema mradi huo umewarahisishia kuyapata maji karibu na kuwafanya wawe safi na afya njema.
Mradi wa maji wa Gereza la kilimo na Mifugo Ushora uliibuliwa mwaka 2017 kupitia Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida kwa kuwasilisha kwa katibu Tawala wa Mkoa.
Mradi huo umeweza kutatua changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji katika eneo la Gereza la Ushora na shule ya Msingi Utemini.
Mkurugenzi wa Mazingira Wizara ya Maji akimtaka Meneja wa RUWASA wilayani Iramba kuhakikisha mradi wa maji Ushora unadumu na unaleta manufaa kwa jamii ya wanaushora, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula na kulia kwake ni Profesa Giuseppe kutoka Italia. Picha na Hemedi Munga
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula akiwa na viongozi mbalimbali eneo la Gereza la Ushora Wilayani Iramba. Kushoto kwake ni Msekwa Omari Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida akifuatiwa na katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Iramba, Ibrahimu Mjanaheri na kulia kwa Mkuu wa Wilaya ni Mkurugenzi wa Mazingira Wizara ya maji Lidya Joseph akifuatiwa na Profesa Giuseppe kutoka Italia. Picha na Hemedi Munga
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.