Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh: Emmanuel Luhahula amefanya ziara ya kutembelea ujenzi na Ukarabati wa Kituo cha Afya kijiji cha Kyalusanga Kata ya Kinampanda.
Katika Ziara hiyo, Mhe: Emmanuel Luhahula Amefanya Mkutano wa hadhara na Wananchi katika eneo la ujenzi wa Kituo cha Afya kilichopo Kijiji cha Kyalusanga. Aidha amewaomba wananchi wa kijiji cha Kyalusanga kuwa na ushirikiano na viongozi wa Kata na Vijiji kuunga Juhudi za Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye alichangia mifuko 600 za Saruji na Nondo 200 kwa ajili kufanikisha zoezi la Ujenzi na Ukarabati wa Kituo cha Afya ili wananchi waweze kupata huduma.
Vilevile Mkuu wa Wilaya ya Iramba Amewaomba Wananchi wa Kata ya Kinampanda Kuweka akiba ya Chakula kwa kuwa mazao mengi yameharibiwa na wadudu na sehemu zingine za Mbuga Mazao yalizama kwa sababu ya Mvua nyingi zilizonyesha pia Mazao mengine yameharibika kwa sababu ya Jua Kali. Kwahiyo hali ya chakula inaweza hisiwe rafiki kwa wananchi na Kuwashauri Wananchi kutuza Chakula cha Kutosha kwa ajili ya familia zao. Vilevile amewashauri kulima Mazao ya Mihogo na Viazi.
Aidha amesisitiza Jamii nzima ya Kata ya Kinampanda kuchangia Chakula kwa ajili ya Wanafunzi kupata chakula wakiwa mashuleni.
Wananchi wa Kata ya Kinampanda wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Iramba
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.