Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel J. Luhahula amekabidhiwa madawati mia moja (100) yenye thamani ya shilingi milioni kumi(10,000,000) kutoka kwa Bwana Nsolo M. Mlozi meneja kanda ya kati wa Benki ya NMB, ambapo madawati hamsini (50) ni ya shule ya Sekondari Lulumba na madawati hamsini (50) ni ya shule ya Sekondari Tumaini.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Iramba ameyakabidhi Madawati hayo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. Linno P.Mwageni kwa ajili ya kuyakabidhi katika shule ya sekondari Lulumba na Shule ya sekondari Tumaini.
Vilvile amemuwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba kuwa Mkandarasi yeyote anayeweza kufanya biashara ya kujenga ni lazima mojawapo ya kigezo kwenye tenda bodi kiwe ni kufungua akaunti kwenye Benki ya NMB katika eneo letu ili kuongeza mapato katika Halmashauri yetu.
Mhe. Luhahula ameshukuru sana Benki ya NMB kwa ushirikiano mkubwa na kutoa michango mbalimbali. “Tunawashukuru kwa kuwa mpo karibu nasi, tunawapenda sana kwa kuwa tunapowahitaji mnakaribia na mkishirikishwa katika majanga mbalimbali mpo tayari kuchangia , sisi wazazini ni vizuri tukawafungulia watoto wetu akaunti za NMB, wanafunzi wetu mpende kuwa na akaunti ili pesa kidogo mnayoiweka mle ni kwa ajili ya kujiwekea Akiba, wananchi tujiunge na NMB, NMB ipo karibu yetu itatusaidia na tiyari tumeona msaada huu,ninakuhakikishia madawati haya uliyoyatoa yatatumika vizuri na utaona ufaulu wa watoto wetu utaongezeka zaidi.”
Ametoa tahadhari kwa watoto, wavulana na wanaume wanaochezea watoto wetu wa shule wakamatwe na kuchukuliwa hatua na nyinyi watoto wa kike endeleeni kujiheshimu, msidanganyike kwa sababu elimu ni msingi na ufunguo wa Maisha, hakuna atakayekusaidia urithi pekee unaoweza kukusaidia katika Maisha yako ni elimu. Amesema Luhahula.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwl. LinnoMwageni baada ya kupokea madawati mia moja (100) yenye thamani ya shilingi milionikumi (10,000,000) toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe, Emmanuel J. Luhahula yaliyotolewa na meneja wa NMB kanda ya kati Ndugu Nsolo M. Mlozi amemuagiza Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Bi Elizabeth J. Lussingu kukabidhi madawati hayo kwa mkuu wa shule ya Lulumba sekondari madawati hamsini (50) na mkuu wa shule ya Tumaini Sekondari Madawati hamsini (50). Amewasisitiza kuyatunza madawati hayo na yawe ni chanzo cha kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.