Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mh. Emmanuel Luhahula pamaoja na Afisa Kilimo wa Wilaya Bi Malyetha Kasongo na Viongozi wengine Kutoka Ngazi ya Wilaya wamefanya ziara ya siku Tatu ya kukagua Kilimo cha Mashamba ya Pamba Kata ya Mtekente Tarafa ya Ndago, Kata ya Mtoa, Kata ya Shelui, Kata ya Mgongo na Kata ya Ntwike Tarafa ya Shelui Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida.
Wamekagua Shamba la Shule ya Msingi Kisonga Hekari 4, Shamba la Shule ya Msingi Mtekente Hekari 6, Shamba la Bwana Nasoro Nafutari Hekari 2, Shamba la Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Ramadhani Panda Hekari 5 Kata ya Mtekente Tarafa ya Ndago.
Pia wamekagua Kilimo cha Mashamba ya Pamba Kata ya Mtoa Tarafa ya Shelui ambapo Kijiji cha Msai kina Jumla ya wakulima wa Mashamba ya Pamba 700 wenye Hekari 9100 zilizolimwa Pamba.
Vile vile Wamekagua Kilimo cha shamba la Bwana Bakari Hamis Hekari 9, Shamba la Mwalimu Hekari 4, Shamba la Abdalla Jumanne Hekari 11/2, Shamba la Bwana Ramadhani Selemani Hekari 71/2, Shamba la Shule ya Msingi Mtoa Hekari 21/2, Shamba la Kikundi cha Muongozo Hekari 11/2 na Shamba la Kikundi Kilichopo Ikungi Hekari 4.
Katika Ziara hiyo, wamekagua Kilimo cha Pamba kwenye Shule ya Msingi Mapinduzi Hekari 4, Shule ya Sekondari Ntwike Hekari 4 , Shule ya Sekondari Shelui Hekari 21/2
Vilevile wamekagua Shamba la Bwana Donald Kiduja Hekari 6, Shamba la Bwana Ezekiel Shuka Hekari 4, Kata ya Ntwike Tarafa ya Shelui.
Pia Wamekagua Shamba la Bwana Edward Kingu Hekari 1, Shamba la Bwana Rashid Juma Hekari 2, Shamba la Bwana Nicholas Makoye Katibu Tarafa Shelui Hekari 2, Shamba la Anfrey Mkumbo Mwenyekiti wa Kijiji Mgongo Hekari 4 na Shamba la Peter Shimo Hekari 2 Kata ya Mgogo Tarafa ya Shelui.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mh.Emmanuel Luhahula ametoa maelekezo kwa Wakulima wote Katika Tarafa zote Kuchukua Pembejeo zinazotolewa bure Mahali zilipo za Kuuwa Vidudu ili waanze kupuliza Mashamba yao Mapema, Pia amewaomba wananchi waliolima Pamba kusaidiana Mabomba yaliyopo ya kunyunyizia dawa kwa sasa wakati serikali ikitafuta ufumbuzi wa Mabomba mengine.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.