Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoani Singida Mhe:Emmanuel Luhahula akiwa kwenye picha ya pamoja na Walimu wa shule za misingi za Wilyani ya Iramba ambao wapo kwenye semina ya Kufundisha na kujifunza kunakozingatia Usawa wa jinsia.
Malengo ya semina ni kujifunza na kutumia mbinu za kufundishia na kujifunzia ambazo zitatoa fursa sawa kwa wanafunzi wote wa kike na wa kiume Mashuleni kushiriki katika mchakato wa kujifunza na kupata mafanikio katika kujifunza kwao.
Mafunzo ya semina hiyo imewajengea Walimu uwezo wa Kufundisha na kujifunza kuzinagatia usawa, Kuheshimiana baina ya Walimu kwa walimu na Wanafunzi kwa Wanafunzi kwa Kutumia lugha nzuri ya Staha na Kurekebisha Matini ambazo hazizingatii usawa wa jinsia.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba amewaomba Walimu kutumia taaluma waliopata kipindi hiki cha Semina ili wakaboreshe Elimu katika maeneo yao. Aidha amewaomba kila moja awajibike ili kuwajengea misingi mizuri ya elimu wanafunzi kwenye masomo yao.
Vile vile amesistiza walimu wahakikisha wanafunzi wanapewa chakula wakiwa Mashuleni ili kuwajengea wanafunzi hao uelewa mzuri akiwa Darasani.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.