Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoani Singida Mhe. Emmanuel Luhahula amefanya kikao na uongozi wa wachimbaji wadogo wadogo wilayani Iramba.
Mhe. Luhahula amewapongeza viongozi hao kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya kwenye shughuli mbali mbali za kujenga wilaya yetu na Taifa letu kwa ujumla.
Lengo lakikao hicho ni kujenga ushirikiano wakaribu na wachimbaji wadogo wadogo ilikudhibiti wizi na uuzwaji holela wa madini ya dhahabu katika maeneo hayo. aliogeza kwa kusema, ushirikiano wetu utarahisisha ukusanyaji wa mapato na kuwasaidia wachimbaji kuuza dhahabu yao kwa bei halisi na kudhibiti walanguzi katika maeneo ya wachimbaji. Aliyasema hayo kwenye Kikao hicho kilichofanyika leo Tarehe 11.10.2018 katika ukumbi wa mkuu wa wilaya ya Iramba ambacho kimeudhuliwa na viongozi wa wachimbaji wadogowadogo wilayani Iramba, viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba na wajasiliamali.
Vilevile alifafanua kuwa utaratibu unaotumiwa na wachimbaji wadogo wadogo kuchenjua dhahabu, umekuwa ukipoteza dhahabu nyingi ikilinganishwa na utumiaji wa njia za kisasa, Pia hakuna kumbukumbu sahihi na taarifa zilizo wazi zinazoonyesha soko halisi la uuzaji wa dhahabu inayochimbwa na wachimbaji wadogo katika maeneo mbalimbali wilayani hapa.
“Tuna wachimbaji wadogo wa dhahabu wengi sana hapa wilayani Iramba, na wanapochimba wanapata dhahabu lakini ukiwauliza wanauza wapi dhahabu yao hakuna majibu sahihi, pia ukiuliza bei kila mmoja anamajibu yake, na kwa mtindo huu wanaikosesha Halmashauri yetu mapato, hali hii haikubaliki lazima idhibitiwe” alisema Luhahula.
wachimbaji wadogo wana wajibu wa kuilinda rasilimali hii ili wanufaike na rasilimali hiyo ya madini hivyo viongozi hao wa wachimbaji wadogo wadogo wilayani Iramba wanajibu wa kuwasisitiza wachimbaji wao kufuata kanuni na sheria za uchimbaji madini ilikuleta maendeleo yenye tija.
Mhe. Luhahula ameagiza viongozi wa wachimbaji wadogowadogo wilayani Iramba kuweka uratibu mzuri wakuuza dhahabu ili kudhibiti wizi na uuzwaji holela wa madini ya dhahabu wilayani hapa.
KIOMBOI, IRAMBA
Anuani ya Posta: P.O BOX 155. KIOMBOI-IRAMBA
Simu: 026 - 2532253
Simu: 026 - 2533001
Barua pepe: ded.irambadc@singida.go.tz
Copyright ©2017 Iramba District Council . All rights reserved.